Mabingwa: Chelsea wakishangilia kombe la vijana chini ya miaka 21 kutoka timu za ligi kuu msimu wa 2013/14
MSIMU huu uongozi wa ligi kuu
unatarajia kuzindua mashindano mapya ya kombe la ulaya kwa timu za ligi
kuu nchini England chini ya miaka 21 na timu kutoka nje ya England.
Vikosi vya vijana chini ya miaka
21 kutoka timu nane (8) za juu katika msimamo wa ligi kuu Engalnd
zikiwemo klabu za Manchester City, Manchester United na Chelsea
vitashiriki pamoja na timu nane (8) kutoka nje ya England ambapo jumla
ya timu itakuwa ni 16.
Hii hatua ni kutekeleza mkakati
maalumu wa soka la vijana ulioanzishwa mwaka 2011 ili kuwaimarisha
vijana wanaozalishwa na klabu za juu za England.
TIMU 16 ZITAKAZOSHIRIKI
Liverpool,
walioshiriki ligi ya vijana chini ya miaka 21 msimu uliopita
hawatashiriki mashindano hayo na badala yake nafasi hiyo imeenda kwa
West Ham waliomaliza nafasi ya tisa katika msimamo msimu uliopita.
Mashindano hayo yataenda sambamba na ligi ya vijana chini ya miaka 21.
Kwa sasa yatawavutia watu wengi zaidi kwasababu Sky Sports na BT Sports watarusha ‘Laivu’ mechi 10.
Waandaaji
wana matumaini kuwa michuano hii itawavutia watu wengi na timu zitapata
wachezaji wao wazuri ili kuwaingia katika timu za wakubwa.
Mkurugenzi
wa akademi ya Schalke ,Oliver Ruhnert alisaidia kuzalisha wachezaji
wanne walioisadia Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka huu na timu yake
itashiriki michuano hiyo ya vijana chini ya miaka 21. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment