RAIS
Mstaafu wa klabu ya Simba Sc Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail
Aden Rage (CCM), ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
amenusurika kifo na kuumia bega la Kushoto akiwa na watu wengine watatu
baada ya gari alilokuwa akitumia kusafiria aina ya Toyota Land Cruser T
845 BQS (gari binafsi) kuacha njia na kuanguka katika eneo la
Chigongwe wakati akiwa njiani kuelekea mjini Dodoma kuanza vikao vya
Bunge la Katiba leo.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Dodoma, David Misime, amesema ajali hiyo imetokea jana Agost 4, 2014 na
kuwa imetokea katika eneo la Njia panda ya Kigwe katika barabara ya
Singida Dodoma, wakati mbunge huyo akielekea mkoani Dodoma kwa ajili ya
kuanza vikao vya Bunge Maalum la katiba.
Amesema Rage, ameumia katika
bega la kushoto na mgongoni huku Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tabora,
Munde Abdalla Tambwe, akiumia sehemu za kichwani na kuwa majeruhi hao
wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Amesema watu wengine waliokuwepo
katika gari hilo ni pamoja na Mwanahamis Athumani, John Hoya ambao wote
kwa pamoja wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo. Hata hivyo amesema chanzo cha
ajali hiyo bado hakijafahamika, na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi
ili kujua chanzo cha ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment