Benki ya Dunia imetangaza kutoa
msaada wa hadi dola milioni mia mbili, kutoka mfuko wa dharura wa
msaada, ili kuzisaidia mataifa matatu ya Afrika magharibi kukabiliana na
ugonjwa hatari wa ebola.
Pesa hizo zitasaidia Liberia, Sierra Leone na
Guinea, ili kuboresha vifaa vya afya ya umma na kushughulikia matatizo
ya uchumi yaliyosababishwa na ugonjwa huo.Rais wa Bank ya Dunia Jim Yong Kim amesema amehuzunishwa sana kwa jinsi Ebola unavyoendelea kuvuruga mfumo wa afya kwa nchi tatu.
Kwa mwaka huu pekee karibu watu mia nane na tisini wamekufa kutokanana Ebola katika nchi za Afrika Magharibi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment