Mapambano ya risasi yaliyodumu
saa tano katika uwanja wa mji mkubwa zaidi nchini Pakistani ,Karachi
yamewauwa watu 23 wakiwemo washambuliaji wote 10.
Washambuliaji hao waliokuwa na silaha nzito
nzito waliingia sehemu ya majengo ya uwanja huo kupitia njia
zinazotumiwa na ndege za mizigo au zile zinazotumiwa kuwapokea wageni
wenye hadhi na sifa yaani V.I.Ps.Walipenya usiku wa manane na kuanza kuwashambulia maafisa usalama kwa gruneti na kwa kuwafyatulia risasi.
Makamanda katika jeshi waliitwa kukabiliana na washambuliaji hao na milio ya risasi ilisikika hadi alfajiri wakati hali ilipodhibitiwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Haijabainika vyema ni akina nani hasa walioshambulia lakini yamewahi kufanyika mashambulio kama hayo hasa katika maeneo ya wanajeshi wa angani na wa majini ambapo wanamgambo wa Taliban walihusika.
Na BBC