Jeneza lenye mwili wa mtoto Nasra Rashid (4) likishushwa kutoka kwenye
gari ili kuingiza katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa
wa Morogoro Hospitali ya Taifa ya Muhimbi jijini Dar es Salaam. Picha na
Juma Mtanda
Ndugu wa baba wa
mtoto, Nasra Mvungi (4) aliyefariki dunia usiku wa kuamkia juzi katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, jana walijitokeza wakitaka wapewe mwili wa
marehemu kwa ajili ya maziko.
Baada ya kuwasili hospitalini hapo saa 1:35
asubuhi, ndugu hao wakiongozwa na baba wa mtoto huyo, Rashid Mvungi
walikutana na maofisa wa ustawi wa jamii wakiongozwa na Ofisa Ustawi wa
Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungatuti wakitaka wakamzike mtoto wao
kwa kufuata imani ya dini yao ya Kiislamu.
Hata hivyo, Ngungatuti alipinga hoja hiyo akisema
suala la ndugu kuzika halina nafasi na kwamba mtoto atazikwa na ustawi
wa jamii ambao ndiyo waliokabidhiwa mtoto huyo na polisi.
“Tutamzika kiserikali kwa kuzingatia imani ya dini
yake lakini hatutawakabidhi maiti kwa namna yoyote,” Ngungatuti alisema
na kuongeza kuwa wanafanya hivyo kwa kufuata misingi ya kisheria.
Akizungumzia suala hilo Mvungi alisema: “Ndugu
zangu wanataka mtoto tupewe lakini kama sheria inakataza mimi sina neno
ila kama ingekuwa ni matakwa yangu ningependa nipewe mwanangu nikazike
mwenyewe.
Sakata hilo liliendelea mjini Morogoro ambako
baada ya mwili kuwasili, watu wanne; wanawake wawili na wanaume walifika
Ofisi za Ustawi wa Jamii na kujitambulisha kuwa ni bibi na wajomba wa
marehemu wakitaka wapewe mwili wa mtoto huyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz