Kiongozi wa Dhehebu la Shia nchini Iraq Moqtada al-Sadr ametoa taarifa akitangaza kujiuzulu kwake katika ulingo wa kisiasa.
katika tangazo ambalo halikutarajiwa na wengi na
ambalo liliwekwa katika mtandao wake,Bwana Sadr amesema kuwa
hatashikilia wadhfa wowote wa serikali wala kuwa na wawakilishi bungeni.Taarifa hiyo pia imesema kuwa atazifunga afisi zake zote isipokuwa zile za kutoa misaada pekee.
Bwana Sadr na wanamgambo wake wa Mahdi walipata ushawishi nchini Iraq baada ya uvamizi wa marekani nchini humo mnamo mwaka 2003.
lakini katika miaka ya hivi karibuni amepoteza umaarufu wake kufuatia mzozo kati yake na waziri mkuu nchini humo Nouri al-Maliki.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz