Sikukuu ya wapendanao inasherekewa kila ifikapo tarehe 14 mwezi wa pili kila mwaka.
Watu wengi wanaosherekea siku hii kwa Nchi za Afrika Mashariki ni vijana walio kati ya miaka 18 hadi 35.
Historia ya sikukuu hii inaanzia miaka mingi jijini, Roma, Italia ikiwa inahusishwa na mtakatifu Valentine au Valentinus aliyekuwa
akiishi jijini humo katika karne hiyo. Wakati wa maisha ya mtakatifu
Valentine Roma ilikuwa ikitawaliwa na Kaisari, Claudius II, ambaye
alipata hisia wakati huo kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule
asiyekuwa na mke wala familia.
Claudius alilifanyia kazi wazo lake na
aliamua kupiga marufuku ndoa zote kwa askari wa nchi hiyo, jambo ambalo
halikukubaliwa na mtakatifu, Valentinus. Hivyo Valentinus alichukua
jukumu la kukaidi amri ile na kuendelea kuwafungisha ndoa kwa siri
maaskari waliokuwa wakitaka kufungishwa ndoa.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Haikuchukua
muda mrefu, taarifa zilimfikia mfalme, Claudius na alipopata habari
hizo aliamuru kukamatwa na kufungwa gerezani na kisha Valentinus aliuawa
kwa amri ya Kaisari. Kuna taarifa zinadai kuwa kabla ya kuuawa kwa
Valentine wakati huo akiwa amefungwa, mtakatifu Valentine aliandika
barua ya salamu kwa binti aliyekuwa amekwenda kumsalimia gerezani. Na
mwisho wa barua kulisomeka maneno yaliyoandikwa ‘From your Valentine’.
Tangu hapo Valentine akawa anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na siku hii ikawa inaadhimishwa duniani kote.
Baada ya kufariki kwa mtakatifu huyo ndipo wananchi wengi duniani wakaamua kuadhimisha siku hii kama sherehe ya kumkumbuka Mtakatifu Valentinus.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz