Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na wahariri wa gazeti la Mwananchi alipotembelea makao makuu ya Mwananchi Communications Limited, yaliyopo Tabata Relini, Dar es Salaam jana.
Kiongozi wa Chama cha ACT -
Wazalendo, Zitto Kabwe amesema zaidi ya wabunge 50 wa vyama mbalimbali
vya siasa nchini watajiunga na chama hicho kipya na kugombea ubunge
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Zitto ambaye alijivua ubunge wa Kigoma Kaskazini
baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema, amebainisha kuwa wabunge hao,
wakiwamo wa CCM na Chadema, ni miongoni mwa watu wanaokichangia fedha
chama hicho kilichopata usajili wa kudumu Mei, mwaka jana na kuzinduliwa
mwezi uliopita.
Pia, amewatangazia vita wabunge wa majimbo manane
ya Mkoa wa Kigoma, akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na ushindi katika
uchaguzi huo ni lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa chama hicho
kimejipanga kuyabeba majimbo yote. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Akizungumza na waandishi wa Mwananchi katika ofisi
za gazeti hili, Dar es Salaam jana, Zitto alisema ACT ni chama
kilichojipanga na ndiyo maana haikuwa ajabu katika mkutano wake mkuu wa
hivi karibuni kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 na kufanya uzinduzi
wa aina yake, huku akisisitiza kuwa chama hicho kinaungwa mkono na watu
wengi.
“Tuna wagombea ubunge wengi wakiwamo wabunge wa
sasa ambao katika Uchaguzi Mkuu Oktoba hawatagombea kupitia vyama vyao
vya sasa. Wapo ambao hawatakwenda hata katika kura za maoni za vyama
vyao na wameshafanya uamuzi,” alisema.
Huku akizungumza kwa kujiamini, Zitto alisema
wabunge hao ndiyo sababu ya chama hicho kuwa na uwezo wa kujiendesha na
kufafanua kuwa ACT kinawakaribisha wabunge na makada wote kutoka vyama
vya Chadema na CCM.
“Wale ambao wanabanwa CCM na kukosa uhuru wa
kuhoji jambo lolote hiki (ACT) ndicho chama chao. Wale ambao wanaamini
kuwa aina za siasa tulizotaka kuzifanya ndani ya Chadema tukashindwa
kuzifanya na wanadhani ni siasa muhimu zinazotakiwa, wapo na sisi,”
alisema.
Kuhusu Kigoma
“Nahitaji majimbo yote ya Kigoma kuchukuliwa na
ACT bila kukosa hata moja na hili hata Serukamba (Mbunge wa Kigoma
Mjini-CCM) analijua. Mwanasiasa anayetaka kuwa mbunge Kigoma lazima aje
ACT,” alisema Zitto ambaye pia alirejea kauli yake kuwa atagombea ubunge
katika jimbo jingine lakini siyo Kigoma Kaskazini.
Kauli hiyo ya Zitto inawagusa wabunge wa sasa wa
majimbo ya Kigoma ambao ni; Felix Mkosamali (Muhambwe), Moses Machali
(Kasulu Mjini), Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) na David Kafulila
(Kigoma Kusini), wote wa NCCR-Mageuzi na Peter Serukamba (Kigoma Mjini,
Christopher Chiza (Buyungu) na Albert Obama (Manyovu) wa CCM.
Alipoulizwa iwapo wabunge hao wa majimbo ya mkoa
huo ni miongoni mwa watu watakaohamia chama hicho alisema, “Sasa huo ni
mtizamo wenu. Ukiwa mwanasiasa lazima uwe na msingi, nataka msingi uwe
Kigoma.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Tutakutana tena kwenye chumba hiki (cha mikutano)
baadaye mwezi Novemba ili mnisute kwa kauli yangu na hapo itakuwa baada
ya matokeo kutoka. Nahitaji kushinda kila kitu.
Nafasi ya CCM
Alisema changamoto iliyopo ni uwezekano wa kupata rais ambaye chama chake kitapata wabunge wachache na hivyo kushindwa kupata waziri mkuu kwa mujibu wa Katiba.
Nafasi ya CCM
Akizungumzia nafasi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu
alisema: “CCM inaweza kuondoka madarakani katika uchaguzi huu. Unajua
chama hiki ilikuwa kiondoke madarakani mwaka 1995 wakati wa (Augustine)
Mrema lakini kulikuwa na (Julius) Nyerere ambaye alikuwa na uwezo wa
kuzunguka na kusema watu waendelee kuichagua CCM.
“Lakini mwaka 2015 Nyerere hayupo na hakuna mwenye
kaliba yake ambaye anaweza kuzunguka na kusema msichague upinzani,
chagueni CCM.
“Katika chaguzi za Serikali za mitaa zilizopita,
CCM ilikuwa ikishinda kwa asilimia 91 hadi 96, lakini katika uchaguzi wa
mwaka 2014 asilimia zimeshuka hadi 75.
Alifafanua kuwa kipindi ambacho CCM ilikuwa
ikipata kura nyingi katika uchaguzi wa mitaa katika ubunge ilikuwa
ikipata asilimia 60.
Akitolea mfano asilimia ya kura za urais za CCM
tangu mwaka 1995 alisema, “Mwaka 1995, CCM ilipata asimilia 61, mwaka
2000 (asilimia 71), mwaka 2005 (asilimia 80) na mwaka 2010 (asilimia
60).
“Kipindi ambacho CCM ilikuwa inapata kati ya
asilimia 90 hadi 96 ya uchaguzi wa mitaa katika ubunge ilikuwa inapata
asilimia 60. Sasa hivi imepata asilimia 75 Serikali za mitaa unategemea
nini katika Uchaguzi Mkuu? Hiki ni kiashiria kwamba hali ni mbaya kwa
CCM.”
Alisema changamoto iliyopo ni uwezekano wa kupata rais ambaye chama chake kitapata wabunge wachache na hivyo kushindwa kupata waziri mkuu kwa mujibu wa Katiba.
“Kuna uwezekano wa kuwa na rais kutoka upinzani na waziri mkuu kutoka CCM.”
Alisema vyama vya upinzani vinaweza kutoa rais
lakini haviwezi kupata viti vingi vya ubunge kwa sababu vyama hivyo
vinapata ushindi zaidi katika majimbo ya mijini na miji midogo ambako
watu wanataka mabadiliko na siyo katika majimbo ya vijijini ambako watu
wanachagua mtu kwa uwezo wake wa fedha na umaarufu wake.
“Jambo hilo likitokea itakuwa ni changamoto ya
kikatiba kwa sababu chama chenye wabunge wengi ndicho kinakuwa na waziri
mkuu, lakini Katiba inasema waziri mkuu anateuliwa na rais.
Rais anatakiwa kumteua waziri mkuu kutoka chama chenye wabunge wengi na Bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais.
Ikitokea hivyo, rais anachoweza kukifanya ni kuvunja Bunge ili kurudi katika uchaguzi,” alisema.
Alisema ili kuepuka jambo hilo, lazima upinzani
umtangaze mtu atakayekuwa waziri mkuu iwapo utashinda jambo ambalo
alisema siyo maarufu katika siasa za Afrika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment