Friday, December 06, 2013
MZEE NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA, TANZANIA KUOMBOLEZA SIKU TATU
Marehemu Nelson Rolihlahla Mandela enzi za uhai wake.
Rais
wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia muda mfupi
uliopita akiwa na umri wa miaka 95 jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amethibitisha taarifa hizo!
Rais Zuma amesema "taifa limepoteza mtu muhimu" na kuongeza "kwa sasa amepumzika. Yupo mahala pema"
Mzee Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu amefariki akiwa amezungukwa na familia yake nyumbani kwake Johannesburg.
Mandela atazikwa kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti alisema Rais Zuma.
Alikuwa
akipatiwa matibabu kwa takribani miaka mitatu iliyopita na hali yake
ilibadilika zaidi katika miezi sita ya mwisho kabla ya kifo chake.
Thursday, December 05, 2013
PAPA FRANCIS ADAIWA KUTOROKA VATICAN USIKU....!!!
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amedaiwa kutoroka usiku Makao Vatican ili apate fursa ya kwenda kutoa misaada kwa walemavu na watu wasiojiweza.
Tetesi za Papa Francis kuwatembelea maskini hao
usiku kwa kujificha zimekuja baada ya mahojiano yaliyofanywa na Askofu
Mkuu, Konrad Krajewski ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya fedha toka
kwa wasamaria wema na kuwapelekea maskini.
Imeelezwa kuwa Askofu Krajewski amekuwa
akiambatana na Papa Francis wakati mwingine na kwenda kuwapa misaada
maskini maeneo ya vijiji, mjini Vatican.
Askofu Krajewski alisema tangu zamani alipokuwa
Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Papa Francis amekuwa akipenda
kwenda mijini nyakati za usiku na kuwatembelea wenye shida mbalimbali.
“Amekuwa akionyesha dalili ya kupenda
kunisindikiza kwenda kuwapa misaada maskini, pindi nikiondoka kwenda
kufanya kazi hiyo,” alisema Padri Krajewski.
MECHI YA NANI MTANI JEMBE KUCHEZWA DESEMBA 21
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro, Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro George Kavishe, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala na
Mkurugezi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba wakioshela alama ya dole
baada ya kutangaza Simba na Yanga kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe
itakayochezwa Desemba 21 jijini Dar es salaam (Executive Solutions)
Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya
Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi,
Desemba 21, 2013 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe
amesema “Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza MECHI YA NANI
MTANI JEMBE (NANI MTANI JEMBE MATCH).
Pambano hili ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Pambano hili ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Kavishe aliongeza kuwa mechi hii ni
maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo imeendeshwa
kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu
zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Wednesday, December 04, 2013
MAMBO YANAYOCHANGIA MUME KUTEMBEA NA HAUSIGELI...!!!
Si ajabu hata wewe unayesoma makala hii aidha umeshawahi kumsikia rafiki kama siyo jirani yako akikorofishana na hausigeli wake au kushuhudia hausigeli akifumaniwa na bosi wake.
Hakika ni matukio ya aibu sana. Inafika wakati unajiuliza inakuwaje mume anamtongoza na hatimaye kutembea na hausigeli wake? Ameshawishiwa na kitu gani au amekosa nini kwa mkewe mpaka anafikia uamuzi huo?
Kimsingi linapotokea tukio kama hili, wengi hujiuliza maswali mengi sana na majibu yake huwa ni magumu kupatikana. Hii ni kwa sababu ni jambo lisilotarajiwa kufanywa na mtu aliyestaarabika. Hata hivyo, tuna kila sababu ya kujua chanzo cha tatizo hili.
Nitajaribu kuzungumzia kipengele kimoja baada ya kingine kuhusiana na yapi yanayotajwa kuwasukuma baadhi ya wanaume kutembea na mahausigeli wao.
Wanawake wanajitakia
Ni jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na baadhi ya watu kuwa, inakuwaje hausigeli anapewa majukumu ya kumhudumia mume wakati mke yupo?
UN: KUTUMIA NDEGE ZISIZO NA RUBANI DRC
Majeshi ya Umoja wa Mataifa katika
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yameanza kutumia ndege zisizo na rubani
kuchunguza harakati za waasi katika mipaka na Rwanda na Uganda.
Hii ni mara ya kwanza kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa kutumia ndege za aina hiyo.
Ndege
mbili za kwanza zilirushwa kutoka mji wa mashariki wa Goma ambao mwaka
jana ulikaliwa kwa muda mfupi na waaasi wa kundi la M23.
Ndege mbili za kwanza zinaundwa na shirika la Italia la Selex ES.
Jeshi la Umoja wa mataifa katika
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ndio kubwa kupita yote duniani na
lilichangia kwa kiasi kikubwa mwezi uliopita ushindi dhidi ya waasi wa
kundi la M23;lakini bado kuna makundi mengine kadhaa ya wanamgambo
nchini humo.
Kikosi kipya kilichoimarishwa nguvu
cha Umoja wa Mataifa kilitumia ndege za helikopta kulisaidia jeshi la
Congo dhidi ya waasi hao wa M23.
Eneo tajiri la madini la mashariki mwa
Congo limekumbwa na vita kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita lakini
kushindwa kwa M23 kumeleta matumaini fulani ya kupatikana utulivu zaidi
kwa eneo hilo.
DK MIGIRO APONGEZWA NA WENGI KWA KUTEULIWA NA RAIS KUWA MBUNGE
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa
Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye
ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa
kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,
Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania
Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,
Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania
Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.
Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.PICHA
NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Tuesday, December 03, 2013
MBOWE, DK SLAA WAPIGWA MARUFUKU KUKANYAGA ARDHI YA MWANZA ...!!!
Mwanza, Tanzania. Gazeti la RAI leo katika ukurasa wake wa kwanza
limeandika kwamba Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Katibu
Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa amepigwa marufuku kukanyaga jijini
Mwanza ambako chama hicho kimepanga kwenda kuwahutubia wananchi.
Mbali na kupigwa marufuku, viongozi wa Chadema wamepewa masharti ya
kufanya kila linalowezekana kumrejesha madarakani aliekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa madaraka.
Viongozi wa Chadema wametakiwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku nne kuanzia jana.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya Chadema, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya Chadema, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele wakati akizungumza na waandishi wa habari.
WAATHIRIKA WA VVU MAKETE WASUSA KUNYWA DAWA ZA ARV
Mkuu
wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akihutubia kwenye maadhimisho ya
siku ya UKIMWI duniani katika kata ya Mbalatse wilaya ya Makete
Wakazi wa Mbalatse wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Makete akitoa hotuba yake
BOKO HARAM WASHAMBULIA NGOME YA JESHI
Wapiganaji wa Boko Haram
Wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia ngome ya Jeshi Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria na kuharibu helkopta mbili maafisa wa serikali
wamesema.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mamia ya wapiganaji wameshambulia
maeneo kadhaa katika mji wa Maiduguri kuanzia mapema asubuhi siku ya
jumatatu.
Amri ya kutotembea ovyo ya saa 24 imetangazwa katika jimbo la Maiduguri.
Na uwanja wa ndege unaotumiwa na wananchi umefungwa kwa muda.
Mwandishi wa habari wa BBC anasema shambulio hilo lililopangwa ni
shambulio kubwa ambalo limerudisha nyumba juhudi za Jeshi la Nigeria.
Maelfu ya watu wameuwawa nchini Nigeria na wapiganaji hao tangu mwaka
2009 wakati Boko Haram walipoanza mashambulizi ya kutaka kusimika
utawala unaoegemea sharia ya kiislamu.
CHADEMA KIGOMA WATOA TAMKO KUHUSU ZIARA YA DR SLAA NA TISHIO LA USALAMA....!!!
Hii ni taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Dec 2 2013 likiwa ni tamko la kikao cha mkoa Chadema Kigoma.
Ni kuhusu Kikao
kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na
Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma
5/12/2013 ambapo
atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya
miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano
ufanyike makao Makuu ya Jimb lengo likiwa ni kuangalia uhai wa chama.
Mambo makuu na muhimu yalizingatiwa ambapo usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.
Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo
i.Mkoa
uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu
kwa mkoa wetu ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uweze
kwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu
ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu
yetu hata kama yanamaumivu ….katiba ifuatwe katika kutatua tatizo –
Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya
k/kuu ambayo dhahiri yalilenga Zitto – Kisiasa.
ii. Mkoa
ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya
viongozi wa majimbo ya mkoa kwamba hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa
kiongozi Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na
wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.
iii. Kwa
hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6
kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara
yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake
Kitaifa.
iv. Hivyo
Mkoa kupitia kikao hicho ikaonekana ni bora kuzuia kuliko kutibu,
tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana
mitazamo ni HATARI katika hali hiyo, mkoa ulijiridhisha usalama
hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo
salama tu.
v. HOFU/TAHADHARI - Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.
Mkoa
hautokwepa lawama na uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini
ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao
Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa
upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa
Taifa.
LENGO KUU: NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA
ALHAJ. JAFARI KASISIKO MSAFIRI WAMALWA
M/KITI MKOA 01/DEC.2013 KATIBU MKOA
Monday, December 02, 2013
MKUU WA MKOA WA MOROGORO MH. JOEL BENDERA NA NAIBU WAZIRI MEDEYE WATUNUKIWA PHD YA HESHIMA
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa
Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu
ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea
matatizo ya Haki za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, (
kulia) mara baada ya kumtunukisha Shahada ya Uzamivu ya Heshima ( PhD)
katika Masuala ya Falsafa ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Califonia State
Christian kilichopo nchini Marekani, kwa mamlaka aliyopewa na Bodi cha
Chuo Kikuu hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akivishwa kofia ya udaktari wa Heshima .
Naibu
Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dk Joel Goodluck Ole
Medeye ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa
Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina
wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki za Binadamu
Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, ( kulia).kati kati kati ni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalongeris.
Subscribe to:
Posts (Atom)