Mwanza, Tanzania. Gazeti la RAI leo katika ukurasa wake wa kwanza
limeandika kwamba Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Katibu
Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa amepigwa marufuku kukanyaga jijini
Mwanza ambako chama hicho kimepanga kwenda kuwahutubia wananchi.
Mbali na kupigwa marufuku, viongozi wa Chadema wamepewa masharti ya
kufanya kila linalowezekana kumrejesha madarakani aliekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa madaraka.
Viongozi wa Chadema wametakiwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku nne kuanzia jana.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya Chadema, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya Chadema, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kwa mujibu
wa Gwanchele, yeye na wenzake wamelazimika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa
wanapinga kitendo cha kuvuliwa madaraka kwa viongozi hao kwa kuwa
Chadema ilichukua hatua hiyo kinyume cha Katiba ya Chama hicho.
“Tutahakikisha tunawaondoa viongozi wote wa ngazi za juu kwa nguvu ya
umma kwani Chadema siyo mali ya mtu binafsi, chama hiki ni cha
wanachama.
“Hatutaki kuyumbishwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi, hao
wanapaswa kukaa pembeni ili kupisha uchunguzi na kama hawataki
kuondoka, nguvu ya umma itawaondoa na ndio maana sisi vijana wa Kanda ya
Magharibi, tumeamua kuwapiga marufuku Mbowe na Dk Slaa kukanyaga Mwanza
kwani wao wameamua kijijengea himaya isiyoguswa katika mikoa ya
Kaskazini, sasa Mwanza wanakuja kutafuta nini,”amesema Gwanchele.
No comments:
Post a Comment