Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa
Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu
ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea
matatizo ya Haki za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, (
kulia) mara baada ya kumtunukisha Shahada ya Uzamivu ya Heshima ( PhD)
katika Masuala ya Falsafa ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Califonia State
Christian kilichopo nchini Marekani, kwa mamlaka aliyopewa na Bodi cha
Chuo Kikuu hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akivishwa kofia ya udaktari wa Heshima .
Naibu
Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dk Joel Goodluck Ole
Medeye ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa
Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina
wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki za Binadamu
Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, ( kulia).kati kati kati ni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalongeris.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Joel Goodluck Ole
Medeye ( kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kulia )
wakiwa katika picha ya pamoja na na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa
Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina
wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki za Binadamu
Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, wa Chuo Kikuu cha Califonia
State Christian kilichopo nchini Marekani, baada ya kuwatunukishaShahada
ya Uzamivu ya Heshima ( PhD) katika Masuala ya Falsafa ya Jamii
,Novemba 30, mwaka huu kutokana na mamlaka aliyopewa na Bodi cha Chuo
Kikuu hicho.Picha na John Nditi, Morogoro
Na John Nditi, Morogoro
MKUU
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera , na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Joel Goodluck Ole Madeye , wametunukiwa Shahada ya
Uzamivu ya Heshima katika Masuala ya Falsafa ya Jamii ya Chuo Kikuu cha
Califonia State Christian kilichopo nchini Marekani.
Bendera
na Medeye walitunukishwa PhD zao ,Novemba 30, mwaka huu na Makamu wa
Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu
ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea
matatizo ya Haki za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki,
kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Bodi cha Chuo Kikuu hicho.
Kabla
ya kuwatunukisha , Profesa Nasioki , alisema moja ya kazi za Vyuo Vikuu
Duniani ni kwenda katika jamii kutafuta watu walionasifa mbalimbali ,
waliobuni na kuchangia maendeleo ya aina mbalimbali katika jamii.
Alisema
, PhD hutolewa hasa kwa watu wale waliotumia muda wao kwa miaka mingi
kusoma , kufanya utafiti wa mambo mbalimbali katika jamii au kiroho na
kupendekeza au kushauri juu ya njia za kuleta mabadiliko yenye manufaa
kwa jamii na hao wanatambuliwa kama wataalamu mbalimbali wahusika.
Hivyo
alisema , Shahada ya heshima hutolewa hasa kwa wale watu ambao
wamatumikia muda na rasilimali zao kubuni na kuchangia michango ili
kutatua matatizo yanayoikumba jamii ,hivyo Chuo hicho kimetambua juhudi ,
elimu , maisha , tabia , utendaji na mchango wa Bendera na Medeye
katika jamii ya Tanzania .
“ Tuko
hapa leo , Nov emba 30 , mwaka huu kwa ajili ya kutunuku shahada ya
heshima kutokana na historiana mchango wenu kwa jamii ya Watanzania”
alisema Profesa Nasioki ambaye ni Mtanzania mbele ya wageni waalikwa
walihudhuria hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Mkoani
Morogoro.
Kwa
mujibu wa Makamu wa Rais wa Chuo hicho,Watanzania 117 wamepata shahada
za aina mbalimbali kutoka Vyuo vya Marekani , Canada na Korea , kati ya
hao watatu wamepata shahada za heshima na tisa shahada za uzamili.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dk Bendera, akizungumza baada ya kutunukiwa PhD,
aliishukuru Bodi ya Chuo Kikuu hicho kwa kutambua mchango wake katika
taifa na kuweza kumtunukia Udaktari wa Heshima.
Hivyo
alisema , kupata PhD ni chachu na changamoto kwake ya kuwatetea
mabadiriko ya kimaendeleo mara mbili zaidi ya utendaji kazi kwa
Watanzania wakiwemo na wananchi wa Mkoa huo.
“ Mtu
asifirikie kutunukiwa PhD sasa nitakweteka la hasha , hii ni changamoto
na kipimo kingine cha kuendeleza kazi ya maendeleo ya wananchi kwa
kushirikiana na watendaji wengine wa Wilaya na mkoa “ alisema Dk
Bendera.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk
Medeye ,alisema , Chuo Kikuu hicho kimetambua uwezo wao na sifa zao ,
hivyo kazi iliyopo mbele ndani ya Wizara kwa kushirikiana na watendaji
wengine ni kujituma kwa bidii na utendaji unaozintatia haki ,taratibu
na sheria.
No comments:
Post a Comment