Friday, December 06, 2013

MZEE NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA, TANZANIA KUOMBOLEZA SIKU TATU

Marehemu Nelson Rolihlahla Mandela enzi za uhai wake.


Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia muda mfupi uliopita akiwa na umri wa miaka 95 jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amethibitisha taarifa hizo!




Rais Zuma amesema "taifa limepoteza mtu muhimu" na kuongeza "kwa sasa amepumzika. Yupo mahala pema"


Mzee Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu amefariki akiwa amezungukwa na familia yake nyumbani kwake Johannesburg.


Mandela atazikwa kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti alisema Rais Zuma.


Alikuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miaka mitatu iliyopita na hali yake ilibadilika zaidi katika miezi sita ya mwisho kabla ya kifo chake.


Mpiganaji huyo wa ubaguzi wa rangi, aliingia Ikulu ya Afrika Kusini akiwa mtu mweusi wa kwanza kuiongoza nchi hiyo mwaka 1994 mpaka 1999 baada ya kutumikia kifungo cha miaka 27 gerezani.
 Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013. Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee nusu mlingoti.
 


Wengine waliotuma salam za rambi rambi ni pamoja na rais Barack Obama wa marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema: "taa kubwa imezimika duniani
"Nelson Mandela alikuwa shujaa"

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...