Friday, December 06, 2013

HISTORIA YA KUSISIMUA YA NELSON MANDELA


JINA KAMILI: Nelson Rolihlahla Mandela
A.K.A: Mandela
MAJINA YA UTANI: Madiba, Black Pimpernel
MAHALI ALIKOZALIWA: Mveso, Transkei, South Africa
KAZI: Mwanaharakati, Kiongozi wa dunia
TAREHE YA KUZALIWA: Julai 18, 1918
TAREHE YA KUFA: DESEMBA 05, 2013
MAHALI ALIKOFIA: Johannesburg, South Africa
ELIMU: Taasisi ya Clarkebury, Chuo cha Wesleyan, Chuo Kikuu Kishiriki cha Fort Hare, Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg.
ASILI YAKE
Nelson Mandela, Mwanasiasa maarufu nchini Afrika Kusini na duniani kwa ujumla ambaye alikuwa mtu muhimu katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi nchini mwake, ni mtoto wa Chifu wa kabila la Tembu, Chifu Henry Mandela. Mandela alizaliwa katika mji mdogo wa Transkei.

CHAMA CHA ANC
Mandela alisoma katika Chuo Kikuu cha Fort Hare na Chuo Kikuu cha Witwatersrand. Akawa mwanasheria mwaka 1942. Mwaka 1944, alijiunga na Chama cha ANC, chama kilichodhamiria kuutokomeza utawala wa makaburu weupe pekee. Mwaka 1960, Chama tawala cha makaburu kilikipiga marufuku cha cha ANC na kuwashitaki viongozi wake kwa kosa la uhaini, lakini Mandela aliachiwa huru.

Rais Barack Obama akiwa ndani ya chumba cha gereza alimokuwa akiishi Mandela akitumikia kifungo chake cha maisha.

KUFUNGWA GEREZANI
Akiendeleza harakati zake za kupambana na makaburu, Mandela alikamatwa, akatiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani kuanzia mwaka 1964 hadi 1990, ambapo maisha yake kama kiongozi wa harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi yakajulikana dunia nzima. Kama mfungwa wa dhamiri, Mandela mara kwa mara alikataa kuachiwa kwa masharti.
Mandela akiwa ndani ya chumba cha gereza alimokaa kwa miaka 26, hapa alikwenda kutembea baada ya kuwa rais
KUACHIWA HURU

Mwaka 1990, akiwa amekaa jela kwa miaka 26 na akiwa na umri wa miaka 71, iliachiwa huru bila masharti yoyote baada ya utawala wa kibaguzi kushinikizwa na jumuiya ya kimataifa. Mwaka 1993, Nelson Mandela alishinda Tuzo ya Nobel kwa harakati zake za kisiasa.
 
Nelson Mandela akiwa na binti yake Princess Zenani Dlamini (kati) wengine ni wajukuu zake Zaziwe Manaway,(kushoto aliyembeba kitukuu chake Ziphokazi Manaway) na Zamaswazi Dlamini (kulia, mwenye kitukuu  Zamakhosi Obiri)
MAISHA YA URAIANI
Mwaka 1994 akiwa katika umri huo, Mandela aligombea kiti cha uraisi na kushinda akiwa raisi wa kwanza mweusi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...