Haya
ni maelezo binafsi ya Mheshimiwa Ester Amos Bulaya bungeni Dodoma
November 4 2013 kuitaka serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya dawa za
kulevya na kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia wahalifu wa dawa
za kulevya.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 28(8) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la
mwaka 2013, napenda kutoa maelezo binafsi ya juu ya tatizo sugu la
uagizaji, uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya linaloongezeka kwa
kasi kubwa nchini, lengo likiwa ni kuitaka serikali ifanye
mabadiliko/marekebisho ya sheria ya Dawa za kulevya na kuanzisha
Mahakama Maalum kushughulikia wahalifu wanaojihusisha na usafirishaji na
biashara ya dawa za kulevya.
Mheshimiwa Spika,
Nimeona ni wakati muafaka kutoa maelezo haya, ili Bunge lako tukufu na Serikali ipate fursa ya kuona uzito wa tatizo hili kutokana na ukweli kwamba katika miaka ya karibuni tatizo la dawa za kulevya katika nchi yetu limeongezeka kwa kasi ya ajabu hali inayopelekea athari kubwa za kiuchumi, kijamii na kiafya. Na mbaya zaidi kundi kubwa linaloathirika ni kundi la vijana, ambao ndio nguvu kazi ya Taifa letu.