UTATA wa risasi umegubika tukio la kifo cha mzazi mwenzake na
mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro, marehemu Anthery Mushi, aliyejiua
kwa kujipiga risasi. Utata huo umeibuka baada ya ndugu wa marehemu
Mushi kushangazwa na kuhoji mazingira ya kifo cha ndugu yao anayedaiwa
kujipiga risasi mbili kidevuni na kupoteza maisha papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Msemaji wa familia hiyo ambaye pia ni kaka wa marehemu, Isaya Mushi alisema familia imebaki kizani juu ya kifo cha ndugu yao na kwamba anayejua siri nzito juu ya kifo hicho ni mzazi mwenzake, Ufoo.
Isaya, alisema mazingira ya kifo cha Mushi ni ya kutatanisha kwani baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi na madaktari, zilitolewa risasi mbili kichwani, huku wakihoji risasi ya pili.
Kwa mujibu wa wataalamu waliobobea katika silaha, ni vigumu mtu kujiua kwa risasi mbili katika eneo la kichwa kwa maelezo kuwa risasi moja inatosha kumaliza uhai wa mtu katika eneo hilo.
“Sisi kama familia bado tukio hili linatupa utata, hivyo tunaomba Jeshi la Polisi litumie busara katika kufanya uchunguzi wa kina kwani, Mushi haiwezekani akajipiga risasi kidevuni ikanasa kwenye ubongo, halafu akajipiga tena kidevuni upande wa kushoto… imetushangaza na hatuelewi tukio hili,” alisema Mushi.
Alisema wanafahamu fika maisha aliyoishi kijana wao kwani alikuwa ni mtaratibu, hivyo maamuzi aliyoyachukua yalikuwa magumu.
“Kijana wetu enzi za uhai wake alikuwa ni mtaratibu, hivyo maamuzi aliyoyachukua yalikuwa ni magumu mno na mwenye siri hiyo ni mzazi mwenzake Ufoo, tuna imani ataeleza,” alisema Mushi.