GWIJI wa Arsenal, Dennis Bergkamp ameelezea nia yake ya kujiunga na dawati la makocha la timu ya Arsene Wenger.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 44
alunga mabao 87 katika miaka yake 11 ya kuchezea Arsenal na amesema
klabu hiyo ina nafasi maalum moyoni mwake.
Robert Pires amekuwa akisaidia
kuendesha mazoezi katika Uwanja wa Gunners, London Colney na Bergkamp,
ambaye aliichezea timu hiyo kuanzia mwaka 1995 hadi2006, anaweza
kuungana naye.
"Hisia alizonazo Johan Cruyff kwa Barcelona, nami ninazo hizo hizo kwa Arsenal," Bergkamp aliiambia Telegraph.
"Nikiwa Arsenal ilikuwa babu kubwa.
Wakati wote nafurahia. Sijawahi kuwa na siku mbaya humo. Ipo katika
fikra zangu wakati wote. Ni sehemu ya malengo yangu kurejea huko.
"Naona kama naweza kuwa sehemu ya makocha. Nafurahia hiyo kazi, hususan kufundisha vitu binafasi kwa washambuliaji,".
Bergkamp alijipatia sifa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka, ubunifu na maarifa ya kisoka alipokuwa Arsenal.
Mchezaji mpya ghali wa Arsenal, Mesut
Ozil amekuwa akifananishwa na Mholanzi huyo, lakini mchezaji huyo wa
zamani wa Uholanzi amesema kila mchezaji ni wa kipekee.
Sasa akiwa kocha Msaidizi wa Ajax, Bergkamp amevutiwa na mwanzo mzuri wa Arsenal msimu huu na kusema Ozil ni kipaji maalum.
"Pamoja na heshima zangu zote kwa
wachezaji wengine wote wa Arsenal, nafikiri ni mmoja ambaye anaweza
kutengeneza tofauti,"alisema.
"Wachezaji wengine ni wazuri katika
kiungo. Lakini unahitaji mtu mmoja fulani wa kiwango cha juu ambaye
anaweza kuhaha Uwanja mzima,". Chanzo: binzubeiry