MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amesema anaweza kuondoka Manchester United ili kusaka timu ambayo atapata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.
Mshambuliaji huyo anayefahamika kama
Chicharito hapewi nafasi kubwa katika klabu ingawa mwezi uliopita
aliifungia timu hiyo bao la ushindi katika Kombe la Ligi, maarufu kama
Capital One dhidi ya Liverpool na zaidi ya mechi hiyo alianza katika
mechi nyingine moja tu, United ikifungwa nyumbani na West Brom.
Hernandez amesema kwamba wakati akiwa
ana furaha kuchezea klabu kubwa kama hiyo, pia anataka nafasi zaidi za
kucheza na anaamini anaweza kuwa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha
kwanza iwe Old Trafford au katika klabu yoyote.
"Nasotea hiyo [kuanza katika mechi zaidi],"alisema Hernandez akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Mexico, Deportes Telemundo.
"Nasotea hiyo [kuanza katika mechi zaidi],"alisema Hernandez akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Mexico, Deportes Telemundo.
"Nafanyia kazi hilo- kupata nafasi
kikosi cha kwanza. Nafahamu kwamba kiwango changu uwanjani kitaniruhusu
kutimiza lengo hilo siku fulani, aidha hapa [Manchester] au popote
katika klabu yoyote.
"Naelekea kutimiza miaka minne hapa
[Manchester United] na kweli, kama ambavyo wakati wote nimesema, nina
furaha kuwa tayari nimechezea moja ya klabu bora duniani, nafanya vizuri
kila siku kutafuta muda zaidi uwanjani,".
"Nahitaji kupewa nafasi zaidi
kuonyesha uwezo wangu, kwa sababu kati yetu sote tunataka kutoa mchango
wetu ili hii timu ishinde ubingwa,".
Hernandez amekuwa akisotea namba
kikosi cha kwanza United kutokana na kuzidiwa kete na akina Wayne
Rooney, Robin van Persie na Danny Welbeck, lakini Mmexico huyo amesema
hiyo inaweza kuwa nzuri kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu England.
"Ushindani ndani ya timu wakati wote
umekuwa mkubwa na ninafikiri hiyo inaisaidia timu kwa kiasi kikubwa, kwa
sababu kuna wachezaji wengi bora ambao kila mmoja kati yao anataka
nafasi kikosi cha kwanza,".
"Mazoezi na mechi zinazokuja
zitatulazimisha kusimama imara kuisaidia timu kuimarika kwa vyote, kwa
uchezaji binafsi na kitimu kwa ujumla,". Chanzo: sportmail
No comments:
Post a Comment