HUU wimbo hatari tupu. Inaelezea maisha ya Diamond kabla hajatoka
kimuziki. Dogo aloimba anadai Diamond ni ndugu yake wa damu na hakumbuki
alipotoka. Duuh kaongea mambo mengi sana. Sina mbavu kwa kweli. Isikilize
hapa Chini. Ni balaa tupu. Ni bonge moja la Ngoma.
Saturday, September 28, 2013
ANGALIA VIDEO YA NDOA YA WATOTO WADOGO HUKO MJINI DODOMA
Vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo katika jamii yetu, huko mkoani Dodoma ilishuhudiwa ndoa ya watoto wadogo kabisa, kiukweli ni ya kushangaza na hata huwezi kuamini, ila ndio mambo ya walimwengu hawa.
ANGALIA VIDEO HAPO CHINI...
Friday, September 27, 2013
MJUE GAIDI SAMANTHA ALYEONGOZA AL-SHABAAB KUUA KENYA
Adaiwa kuuawa Westgate
*Alifika Tanzania kwa Pasipoti ya Afrika Kusini
*Alifika Tanzania kwa Pasipoti ya Afrika Kusini
Ssamantha Lewthwaite, mwanamke wa Uingereza anayetajwa kuwa kiongozi wa ugaidi uliofanyika Nairobi, Kenya
WAKATI umwagaji wa damu katika kituo cha biashara cha Westgate ukiingia siku ya nne jana, Mwanamke ambaye ni raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite (29), anayetajwa kuwa ndiye aliyeongoza kundi la Al-Shabab kufanya shambulizi hilo, anahofiwa kuuawa.
Gazeti la Daily Mail la Uingereza, lilikariri vyanzo vyake vilivyoko ndani ya Jeshi na mfumo wa usalama nchini Kenya, ambavyo vimethibitisha kuwa mwanamke huyo ni miongoni mwa magaidi waliouawa na Serikali ya Kenya.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, katika mahojiano yake na kituo cha habari cha PBS, hakusema kama mwanamke huyo ameuawa lakini alithibitisha kuwa miongoni mwa magaidi waliovamia Westgate ni mwanamke wa Uingereza ambaye hata hivyo hakumtaja jina.
Hatua hiyo iliibua tetesi kwenye vyombo vya habari vya Kenya ambavyo vilimtaja mwanamke huyo kuwa ni Samantha.
Hata hivyo kauli hiyo ya Waziri huyo inaonekana kupingana na ile iliyotolewa awali na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Kenya, ambaye alisema kuwa magaidi wote waliovamia kituo hicho walikuwa wanaume na kwamba huenda baadhi yao walivalia mavazi ya kike.
TAARIFA YA JKT KWA VIJANA WANAOTAKA KUAHIRISHA MAFUNZO
1. Barua binafsi kuomba kuahirisha mkataba iwe na picha yake.
2. Nakala ya barua ya kucahguilwa kujiunga na chuo (Joining instructions)
3. Barua hiyo ieleze kuwa utajiunga na JKT baada ya kuhitimu masomo.
4. Barua zao zifike Makao Makuu ya JKT kabla ya tarehe 02 Kotoba, 2013.
ANGALIZO
Kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ni lazima. Hivyo ni wajibu wa kila mhitimu kuhudhuria mafunzo hayo.
Agizo hili limetolewa na Jeshi la Kujenga Tafia, Makao Makuu.
---
Imetolewa kwenye tovuti: http://jkt.go.tz/mkataba-jkt.html
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2g4C18z5v
2. Nakala ya barua ya kucahguilwa kujiunga na chuo (Joining instructions)
3. Barua hiyo ieleze kuwa utajiunga na JKT baada ya kuhitimu masomo.
4. Barua zao zifike Makao Makuu ya JKT kabla ya tarehe 02 Kotoba, 2013.
ANGALIZO
Kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ni lazima. Hivyo ni wajibu wa kila mhitimu kuhudhuria mafunzo hayo.
Agizo hili limetolewa na Jeshi la Kujenga Tafia, Makao Makuu.
---
Imetolewa kwenye tovuti: http://jkt.go.tz/mkataba-jkt.html
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2g4C18z5v
KENYA YAMSAKA SAMANTHA LEWTHWAITE
Polisi wa kimataifa Interpol,
wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini
Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu
wanaosakwa sana duniani.
Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.
Bi Lewthwaite, mwenye umri wa
miaka 29, ni mjane wa mlipuaji aliyefanya shambulizi la kujitoa mhanga
mjini London Uingereza mwezi Julai mwaka 2005
Anajulikana kama "white widow", na amehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi wa Interpol hata hivyo
hawakuhusisha hatua ya kumsaka Samantha na shambulizi la kigaidi dhidi
ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi lililowaua watu 67.
Hata hivyo, hatua hii ya kumsaka Bi Lewthwaite inakuja punde baada ya shambulizi hili la kigaidi nchini Kenya.
Al-Shabab ilikiri kufanya mashambulizi
hayo yaliyotokana na kutekwa kwa jengo la Westgate na kisha kutekwa kwa
raia wa kawaida waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Kwa mujibu wa polisi wa Interpol,
mwanamke huyo anasakwa na serikali ya Kenya kwa kumiliki mabomu na
kupanga njama ya kufanya mashambulizi kuanzia Disemba mwaka 2011.
Ikiwa mwanamke huyo atakamatwa katika
nchi mwanachama wa Interpol, atazuiliwa na kusibiri kupelekwa katika
nchi anayotakikana kwa kesi kufunguliwa dhidi yake.
Bi Lewthwaite anajulikana kwa jina
bandia la, "Natalie Webb" –na alikuwa anasakwa kwa madai ya kumiliki
hati bandia ya usafiri nchini Afrika Kusini.
Ni mjane wa Germaine Lindsay, mmoja wa
washambuliaji wanne waliohusika na shambulizi la kigaidi mjini London
ambapo watu 52 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa.
Chanzo:
bbcswahili
Thursday, September 26, 2013
BAADA YA KENYA SASA AL-SHABAAB YAIGEUKIA TANZANIA....WATISHIA KUIVAMIA MUDA WOWOTE
*Yajigamba kufanya mashambulio muda wowote
*Watanzania wapewa mafunzo ya ugaidi nje ya nchi
*Polisi nchini wasema vyombo vya ulinzi viko macho
*Mtanzania akamatwa Kenya akihofiwa gaidi
WAKATI wananchi wa Afrika Mashariki wakijawa na hofu ya mashambulio yanayopangwa kufanywa na vikundi vya ugaidi vya Al Qaeda na Al Shabab, imebainika kuna Watanzania waliopewa mafunzo ya ugaidi wanaojiandaa kufanya maovu.
Hayo yamebainika siku chache baada ya wanamgambo wa kundi la Al Shabab kufanya mashambulio katika Jengo la Biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya 70 na kuacha mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa.
Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliyasema hayo jana katika mahojiano maalumu na MTANZANIA.
YAFAHAMU MAJINA YA ASILI YA BAADHI YA MASTAR WA BONGO MOVIES
KWA kawaida binadamu yeyote huzaliwa na kubatizwa jina ambalo hulitumia katika masomo na hata kazi yake.
Tofauti na ilivyo katika fani nyingine, wasanii wamekuwa wakijibatiza majina ya ziada (a.k.a). Mbaya zaidi, majina hayo huwa yanaanza kama utani lakini inafika wakati msanii husika
analizoea jina hilo jipya na kulifanya kuwa kama rasmi. Leo Amani linakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao majina waliyopewa na wazazi wao ‘yamekufa’, hawayatumii kabisa: LULU
Jina lake halisi ni Elizabeth Michael, Lulu lilizoeleka kupitia tasnia ya uigizaji. Alianza kulitumia wakati alipojiunga na Kundi la Sanaa la Kaole.
Hadi leo hii, siyo rahisi kabisa mtu kutokea na kumuita jina la Elizabeth, wengi wanamfahamu kwa jina la Lulu.
RAY
Ray ndiyo jina ambalo limezoeleka na wengi. Vincent Kigosi alilopewa na wazazi wake ni kama limekufa. Kwa zaidi ya miaka kumi sasa tangu alipokuwa kwenye Kundi la Sanaa la Kaole hadi sasa.
Jina la Ray ndiyo watu wanalolifahamu zaidi ingawa hivi karibuni baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa wakijaribu kumuita Vincent ili kurudisha uhai wa jina hilo.
JOHARI
Jina lake halisi ni Blandina Chagula. Johari lilizaliwa kwenye Tamthiliya iliyobeba taito ya jina hilo. Akiwa katika Kundi la Kaole, alianza kujiita Blandy, baadaye alibadilisha jina hilo na kuwa Johari walipoingiza tamthiliya hiyo ambayo pia ilizaa filamu.
MWANAFUNZI AMCHINJA MWALIMU WAKE DARASANI...!!!
KUSHOTO: Mwalimu Sun Wakang. KULIA: Damu ikiwa imetapakaa darasani muda mfupi baada ya tukio hilo. |
Mwanafunzi wa China amemchinja mwalimu wake katika kulipiza kisasi baada ya simu yake ya mkononi kutaifishwa.
Mwanafunzi
huyo, aliyetajwa kwa jila la Lei katika taarifa za habari za mjini humo,
alibambwa na mwalimu wake, Sun Wakang akiwa anachezea simu wakati wa
somo la Kemia katika shule moja mjini Fuzhou, mashariki mwa jimbo la
Jiangxi nchini China.Siku iliyofuata Lei alikwenda kwenye darasa analofundisha Sun ambako mwalimu huyo alikuwa ameketi akisahihisha mitihani, na kumchinja kutokea kwa nyuma.
Mwalimu huyo mwenye miaka 32 ambaye ni baba wa watoto watatu alifariki papo hapo huku mwanafunzi huyo akitokomea kusikojulikana.
Jana Lei alipiga namba ya simu ya dharura na kukiri kuhusika na uhalifu huo kabla ya kujisalimisha mwenyewe polisi mjini Shanghai.
Sun alifanya kazi kama mwalimu wa Kemia katika Shule ya Kati ya Linchuan No. 2 kwa miaka mitano kabla ya mauaji yake ya kutisha, ofisa wa shule Xiong Hainshuo alieleza.
NI AL-QAEDA, SI AL SHABAAB
- Magaidi wa Marekani, Uingereza, Syria wahusika
SHAMBULIO la kigaidi lililofanywa
nchini Kenya Jumamosi iliyopita na watu waliodhaniwa kuwa wafuasi wa Al-
Shabab, sasa limeelezwa kutekelezwa na mtandao mpana zaidi wa kigaidi
wa kundi la Al-Qaeda.
Baadhi ya wachambuzi na wachunguzi wa
masuala ya kiusalama na kimataifa, wameyataja mambo matatu ambayo
yanathibitisha pasipo shaka kwamba waliotekeleza tukio hilo la kuvamia,
kuteka nyara na kuua watu wapatao 68 katika Kituo cha Biashara cha
Westgate, ni wa aina ya kundi ambalo kinadharia na kimatendo linafanana
na lile la kigaidi duniani la Al-Qaeda. Mambo yanayotajwa na wachambuzi
na wachunguzi hao ni pamoja na mbinu, teknolojia na aina ya watu
waliotumika kutekeleza shambulio hilo.
Katika uchambuzi wao, wameeleza kuwa
mbinu iliyotumiwa na magaidi hayo kuvamia pasipo kujulikana mara moja na
vyombo vya ulinzi na usalama vya nchini Kenya, lakini pia aina ya
silaha walizokuwa nazo, inaonyesha kuwa kundi hilo limeamua kutumia
kivuli cha Al-Shabab kufikisha ujumbe kwa dunia kwamba lipo licha ya
uongozi wake kubadilika.
Kwamba mbali na mbinu pamoja na
teknolojia, pia aina ya watu waliohusika kutekeleza shambulio hilo ambao
wamebainika kutoka katika mataifa mbalimbali duniani, ndio ambao
wamewafanya wachambuzi na wachunguzi hao waanze kupata shaka kwamba
huenda kuna kundi kubwa zaidi lililotekeleza shambulio hilo, ambalo
limejivika taswira ya Al-Shabab.
MANJI AWATULIZA WACHEZAJI YANGA
MWENYEKITI wa Yanga SC, Alhaj Yussuf Mehboob Manji amewaambia wachezaji wa timu hiyo kwamba hana matatizo nao kwa matokeo ya awali ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na amewataka waelekeze nguvu zao katika mechi zijazo.
Yanga imeambulia pointi sita
katika mechi tano za awali za Ligi Kuu ya Vodacom, kutokana na sare
tatu, kushinda moja na kufungwa moja, hivyo kuachwa kwa pointi tano
kileleni na wapinzani wao wa jadi, Simba SC.
Jana Manji alikutana kwa chakula
cha jioni na wachezaji wa timu hiyo katika hoteli ya Serena, Dar es
Salaam akiwa ameambatana na Makamu wake Mwenyekiti, Clement Sanga,
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Isaac Chanji na Mjumbe wa Sekretarieti,
Patrick Naggi.
Katika kikao hicho, Manji aliwaambia
wachezaji wa Yanga hamlaumu yeyote kwa matokeo hayo, kwani ligi bado
mbichi, ila akawataka waunganishe nguvu zao kuelekea mechi zijazo, ili
kurejesha ushindi na furaha klabuni.
Pamoja na hilo, Manji alizungumzia suala la madai ya baadhi ya
Pamoja na hilo, Manji alizungumzia suala la madai ya baadhi ya
wachezaji ya fedha za usajili na
akaliweka sawa kwa wale ambao walikuwa wanadai kuwawekea utaratibu wa
malipo haraka, jambo ambalo Naggi ametakiwa kuhakikisha analishughulikia
mara moja.
M23 WAHOFIWA KUJIFICHA MAKANISANI DAR
WASIWASI umeibuka miongoni mwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kuhusu uwepo wa makamanda wa wapiganaji wa kikundi cha waasi wa M23, ambao wamejipenyeza nchini kwa kivuli cha kuendesha shughuli za kihoro katika baadhi ya makanisa.
Duru za uchunguzi zimeonyesha kuwa
baadhi ya watu walioingia nchini kwa mwamvuli wa uchungaji wakitokea
nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, majina yao yamo kwenye orodha
ya wapiganaji wa kikundi hicho cha waasi.
Taarifa mbalimbali zilizokusanywa na
gazeti hili zimeonyesha kuwa, raia hao wa Kongo mbali na kufanya kazi za
kiroho, pia wanajihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na
kufanya biashara ndogo ndogo.
Baadhi ya wachungaji waliozungumza Jumatano kuhusu suala hilo, walishindwa kukubali au kukanusha kuhusu taarifa hizo.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la
Mikocheni B, Assemblies of God, Getrude Lwakatare, ambaye pia ni Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro (CCM), alipoulizwa kupitia simu yake ya
kiganjani iwapo anazo fununu za uwepo watu wa aina hiyo ambao kwa kiasi
kikubwa wameanza kujenga taswira mbaya katika baadhi ya makanisa, alikaa
kimya kwa muda kisha akakata simu.
PAPA BENEDICT AKANUSHA KUTOKUWAJIBIKA KWA KASHFA ZA KANISA.
Papa wa zamani Benedict ameibuka kutoka kwenye ukimya binafsi ndani ya Vatican na kukanusha hadharani kwamba alificha vitendo vya manyanyaso ya kingono kwa watoto na mapadri wa kanisa katoliki.
Katika barua ndefu kwa mtunzi wa
vitabu wa Italia asiye na dini na mwanamahesabu (Piergiorgio Odifredi)
na kuchapishwa jana Jumanne na gazeti la La Republica , Benedict alikana
kutokuwajibika kwa kashfa ya ngono kwa watoto.Lakini amesema kanisa
lazima lifanye kila iwezalo kuzuia vitendo kama hivyo kutokea tena.
Makundi ya waathirika wamemshutumu
Papa huyo kwa kutokufanya vya kutosha kuzuia manyanyaso hayo, kabla ya
kuwa Papa na baada , wakati alipoongoza ofisi ya kanuni ya Kanisa,
ambayo ilihusika na kesi za manyanyayaso.
ALL HAIL FOR THE KING "HE'S BACK" - HUU NDIO UJIO MPYA WA CPWAA
Mashabiki wake hupendelea kumuita "King of BongoCrunk"....jina halisi ni Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa! Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ambaye baada ya ukimya mrefu sasa kuachia kazi zake mpya.
C.P a.k.a CPwaa mwenye tuzo 3 za
Tanzania Kilimanjaro Music Awards na Multiple Channel O Africa Music
Video Awards nominations anakuja kivingine kabisa mwaka huu. Tarehe 1
mwezi wa October 2013, CPwaa ataachia single yake mpya na ya kwanza
kabisa kwa mwaka huu.Single hiyo iitwayo "Chereko Chereko" yenye mahadhi
ya AfroDance imefanywa chini ya studio za 'De Fatality Music" na
producer "Mesen Selekta" ambaye mwaka huu alichukua tuzo ya mtayarishaji
bora Tanzania anayechipukia.Nyimbo hii itapatikana kwenye mitandao yote
na media zote kuanzia tarehe moja October.
Subscribe to:
Posts (Atom)