Wednesday, July 10, 2013
KASEJA ANAWINDWA KILA KONA, USIKU NA MCHANA
KLABU
za APR ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya zipo katika harakarti za kumwania
aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Simba, Juma Kaseja,
imefahamika.
Habari
za uhakika ambazo Sports Lady Blog imezinyaka zinasema viongozi wa timu
hizo wameshaanza mazungumzo na Kaseja ili kumsajili kwa msimu ujao katika nchi
hizo.
Mdau
mmoja wa soka ambaye yupo karibu na uongozi wa timu hizo, alidokeza jana kwamba,
kwa nyakati viongozi wa timu hizo mbili, wamekuwa kwenye harakati za kumsaka
Kaseja, wakiamini bado ni kipa mwenye uwezo mkubwa
langoni.
Licha
ya kutemwa kwenye kikosi cha Simba kwa msimu ujao, Kaseja bado kipa namba moja
wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha wake Kim Poulsen, raia
wa Denmark.
Habari
zaidi zinasema, klabu ya APR iliyofika fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashabiki
na Kati-Kagame Cup na kufungwa na Vital’o wiki moja iliyopira nchini Sudan,
inapewa nafasi kubwa ya kumpata kipa huyo.
Hayo
yanatokea huku Kaseja akiwa kwenye kambi ya timu ya Stars inayojiandaa na mechi
ya kuwania tiketi ya Fainali za Afrika kwa Nyota wa Ndani –CHAN dhidi ya Uganda
itakayopigwa Julai 13, Uwanja wa Taifa Dar es
Salaam.
“Ujue
baada ya Simba kutangaza kuachana na Kaseja, kuna timu nyingi hasa za nje
zimeonesha nia ya kutaka kumsajili lakini mpaka sasa ni APR na Gor Mahia ndio
wako makini zaidi na mchakato huo,” kilisema chanzo hicho.
HUYU NDIE MWIGIZAJI WA HOLLYWOOD ALIYEMTUKANA OBAMA NA MKE WAKE
Anaitwa
Amanda Bynes ni mwigizaji maarufu HoolyWood. Wiki chache zilizopita
alikua katika vita ya maneno na msanii Rihana kupitia mtandao wa
twitter, sasa vita hiyo kaihamishia kwa Raisi wa nchi yake Obama pamoja
na mke wake.
Katika tweet aliyoandika jana alisema “Barack Obama and Michelle Obama are Ugly” na mda mchache tu baada ya kuandika hivyo watu walianza kumshambulia kwa kumwambia kua alichofanya si kitu kizuri kabisa. Pia katika kuonyesha kua watu hawamungi mkono wengi wa followers wake walimunfollow.
Hii si mara yake ya kwanza kuwaita watu weusi ugly kwani alishawahi kumuita na Drake jina hilo
Katika tweet aliyoandika jana alisema “Barack Obama and Michelle Obama are Ugly” na mda mchache tu baada ya kuandika hivyo watu walianza kumshambulia kwa kumwambia kua alichofanya si kitu kizuri kabisa. Pia katika kuonyesha kua watu hawamungi mkono wengi wa followers wake walimunfollow.
Hii si mara yake ya kwanza kuwaita watu weusi ugly kwani alishawahi kumuita na Drake jina hilo
MWANAMKE APEWA MIMBA NA MAITI, ALIJIFANYISHA MAPENZI WAKATI ANAMUOGESHA.
Mwanamke
mmoja mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti ameushangaza ulimwengu kwa
kitendo chake cha Kujilazimishia mapenzi kutoka kwa mwanaume ambaye
amekufa hadi kufikia kupata Ujauzito.
Felicity
Marmaduke (38), Mkazi wa Lexington Missouri, alikumbwa na mkasa huo
baada ya kumtamani marehemu huyo wakati wa kumuosha na ndipo alipoamua
kujiweka juu yake na kuanza kufanya naye mapenzi, cha kushangaza ni
kwamba maiti hiyo iliweza kutoa mbegu za kiume.
Baada ya wiki mbili, mwanamke huyo alienda kujipima ujauzito baada ya kujihisi tofauti na ndipo alipogundua ya kwamba ameshika mimba.
Baada ya wiki mbili, mwanamke huyo alienda kujipima ujauzito baada ya kujihisi tofauti na ndipo alipogundua ya kwamba ameshika mimba.
Ilimbidi
atoe taarifa kwa familia husika ambayo ilimfungulia mashataka kwa
kitendo chake hata hivyo naye amefungua mashtaka akidai iuzwe moja ya
nyumba ya marehemu huyo ili alipwe gharama za matunzo.
MCHUNGAJI AKAMATWA KWA KOSA LA KUUPINGA USHOGA NA USAGAJI.
Tonny
Miano ni Mchungaji kutoka nchini mMarekani ambaye alikwenda Nchini
Uingereza katika Kufanya Mahubiri Huko. Kilichomkuta kilisababishwa na
yeye kusema ya kwamba tabia za kishoga na kisagaji ni Dhambi na
hazimvutii Mungu,.
Polisi
walipigiwa simu na mwanamke mmoja aliyekuwa eneo la tukio akilalamika
ya kwamba hajafurahishwa na maneno anayoongea Tonny, ambaye ni askari
mstaafu wa jeshi la polisi nchini Marekani.
Tuesday, July 09, 2013
MBONA MAJANGAAA....!!! AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI
HATIMAYE wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya Afrika kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..
Mabinti
hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya
zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza
na mwandishi wetu jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na
Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika
wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda
Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE) ambaye
alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana
hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa
mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado
wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.
CHELSEA WAANDAA DAU LA JUU ZAIDI KUMSAJILI ROONEY....!!!
Anasakwa
vibaya sana: Chelsea wameamua kutuma ofa kwa David Moyes ingawa
alitangaza kuwa hafanya biashara, lakini wakali hao wa darajani
wanamhitaji jembe Wayne Roonye
Atabaki au ataondoka? Maisha ya baadaye ya Rooney katika klabu yake ya Manchester United bado hayajulikani
Kocha mpya wa United: David Moyes amesema hamuuzi Rooney kwa sasa
Karibu tena Jose: Malejendari, Frank Lampard na John Terry wamefurahi kuona ujio wa Mourinho katika klau yao ya Chelsea
WAKATI MZEE MANDELA AKIENDELEA KUPATA MATIBABU FAMILIA YAKE WAZIDI KUTIBUANA
Mandla Mandela aendelea kulikoroga
WAKATI
mgogoro kati ya watoto wa Mandela na wajukuu ukizidi kutokota kuhusu
uhalali wa uchifu wa Mandla Mandela, yeye amejibu mapigo akisema Mfalme
Buyelekhaya Dalindyebo wa kabila la abaThembu ”hana akili timamu”.
Hiyo
inatokana na madai yaliyotolewa na mfalme huyo kwamba Mandla hakuwa
chifu sahihi wa ukoo wa Madiba. Alidai kwamba hakukuwa na cheti chochote
halali kilichotiwa saini wakati mandla alipotawazwa kuwa chifu mwaka
2007 – sherehe ambazo zilisimamiwa na Mandela mwenyewe.
Gazeti
la Mail & Guardian wiki iliyopita liliripoti kuwa uchifu wa Mandla
ulilalamikiwa kabla ya Mandela kulazwa hospitalini, ikielezwa kama kweli
anafaa kuendelea kuwa chofu ikizingatiwa kuwa mama na baba yake
walimzaa bila kuoana.
Mgogoro
unaoendelea hivi sasa kati ya Manla na shangazio yake, Makaziwe
Mandela, na wanafamilia wengine unaonekana kama kichocheo kwa baadhi ya
wanafamilia hiyo ambao wangetaka Mandla avuliwe uchifu.
WEMA SEPETU ANASAKWA NA POLISI BAADA YA KUMTUKANA MENEJA WA HOTELI WAKATI YUKO POMBE...!!!
Msanii
wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu
anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za
kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi
meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa
tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo iliyopo Kawe Beach,
jijini Dar.
Akizungumza
na mwandishi wetu , meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa
nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa
ameongozana na marafiki zake wapatao kumi.
Meneja
huyo akaendelea kusema, ilipofika saa tano usiku, Wema na marafiki
zake walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga
kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo.
Aliongeza
kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake,
aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa
makusudi huku meneja huyo akishuhudia.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Akutana na Waandishi Wa Habari Nakutoa maamuzi ya Kamati ya Ushauri (RCC) ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa mpya Mkwajuni Wilayani Chunya.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa Mbeya akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya
wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mbeya akiongea na waandishi wa habari.Picha na Habari na Mdau Joseph Mwaisango
--
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya
hatimaye yatoa ufafanuzi na kupigilia Msumari maamuzi ya Kamati ya Ushauri
(RCC) ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa mpya Mkwajuni Wilayani Chunya.
"NGUVU YA UMMA" INAVYOGHARIMU UHAI WA WAMISRI...!!!
Miili ya wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri ikiwa imehifadhiwa
MAAFISA wa Afya Misri wamesema takriban watu 42
wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo
wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi walikua
wamekusanyika na wanaamini anazuiliwa hapo. Watu wengine 300
wamejeruhiwa.
Kundi la Muslima Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia.
Brotherhood imelaumu jeshi kwa kuwaua raia wake.
Katika kikao na waandishi wa habari, wafuasi hao walimlaani vikali mkuu wa jeshi Abdel Fattah Al-Sisi na kumtaja kama muuaji aliyewashambulia raia wenzake.
Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.
NDEGE YA RAIS WA SOMALIA 'YASHIKA MOTO'
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mahamud
*******
NDEGE iliyokuwa inambeba rais wa
Somalia, imelazimika kutua kwa dharura mjini Mogadishu baada ya moja ya
mabawa yake kushika moto. (HM)Rais Hassan Sheikh Mohamud, alielezea kuwa rais hakujeruhiwa lakini wazima moto walifanya kila hali kuzima moto huo.
Bwana Mohamud alichaguliwa kama rais wa Somalia mwaka jana katika mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa, katika hatua za kumaliza vita vya miaka mingi.
Mwandishi wa BBC Mohamed Mwalimu, alisema kuwa magurugumu ya ndege yaliharibiwa vibaya baada ya tukio hilo.
Rais alikuwa anaelekea katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, wakati ndege hiyo ilipolazimika kurejea Mogadishu.
Moja ya ripoti zilizotolewa za mwanzo kuhusu tukio hilo, ilitoka kwa akaunti ya Twitter ya kundi la al-Shabab lakini haikusema kama imeshambulia ndege hiyo.
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika pamoja na wale wa Somalia, wanaounga mkono bwana Mohamud wamewaondoa wapiganaji wa al-Shabab kutoka mji mkuu Mogadishu, mwaka jana ingawa kundi hilo bado hufanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kuvizia.
Serikali mpya ni ya kwanza kwa zaidi ya miaka 10 kutambuliwa na serikali ya Marekani na shirika la fedha duniani (IMF).
Chanzo: bbcswahili
Monday, July 08, 2013
RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AWAASA WAISLAMU NCHINI
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amewataka Waislamu wote nchini kuishi na Watanzania wenzao katika misingi ya kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana, kama Uislamu ulivyofundisha.
Dk
Shein aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa msikiti wa Masjid Taqwa,
uliopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam, katika hotuba ilyosomwa kwa
niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk Mwinyihaji MakameKatika hotuba hiyo ya ufunguzi wa msikiti
huo, Dk Shein alisema kuwa ni wajibu kwa Waislamu kufanya kila jitihada
katika kuilinda amani na utulivu alioubariki Mwenyezi Mungu hapa
Tanzania.
Alisema kuwa kuna kila sababu kwa Waislamu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba wanaweza kufanya ibada zao katika mkusanyiko mkubwa kama huo wa ufunguzi wa msikiti bila ya hofu, woga wala bughudha ya namna yoyote.Dk Shein alipongeza jitihada zinazochukuliwa na wasimamizi wa msikiti huo katika kuimarisha na kuitunza historia yake tangu ulipoanzishwa mnamo mwaka 1927, ambapo historia hiyo inadhihirisha kuwa msikiti huo ni miongoni mwa misikiti mikongwe katika Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kuwa kuna kila sababu kwa Waislamu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba wanaweza kufanya ibada zao katika mkusanyiko mkubwa kama huo wa ufunguzi wa msikiti bila ya hofu, woga wala bughudha ya namna yoyote.Dk Shein alipongeza jitihada zinazochukuliwa na wasimamizi wa msikiti huo katika kuimarisha na kuitunza historia yake tangu ulipoanzishwa mnamo mwaka 1927, ambapo historia hiyo inadhihirisha kuwa msikiti huo ni miongoni mwa misikiti mikongwe katika Jiji la Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)