Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amewataka Waislamu wote nchini kuishi na Watanzania wenzao katika misingi ya kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana, kama Uislamu ulivyofundisha.
Dk
Shein aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa msikiti wa Masjid Taqwa,
uliopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam, katika hotuba ilyosomwa kwa
niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk Mwinyihaji MakameKatika hotuba hiyo ya ufunguzi wa msikiti
huo, Dk Shein alisema kuwa ni wajibu kwa Waislamu kufanya kila jitihada
katika kuilinda amani na utulivu alioubariki Mwenyezi Mungu hapa
Tanzania.
Alisema kuwa kuna kila sababu kwa Waislamu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba wanaweza kufanya ibada zao katika mkusanyiko mkubwa kama huo wa ufunguzi wa msikiti bila ya hofu, woga wala bughudha ya namna yoyote.Dk Shein alipongeza jitihada zinazochukuliwa na wasimamizi wa msikiti huo katika kuimarisha na kuitunza historia yake tangu ulipoanzishwa mnamo mwaka 1927, ambapo historia hiyo inadhihirisha kuwa msikiti huo ni miongoni mwa misikiti mikongwe katika Jiji la Dar es Salaam.

Alitoa
wito katika kushirikiana kuulinda na kuuendeleza msikiti huo wenye
historia kubwa na kutoa shukurani kwa Yusuph Khamis Yusuph kwa busara
aliyochukua ya kutumia sehemu ya kipato alichojaaliwa kwa kuisimamisha
nyumba hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Dk
Shein alitumia fursa hiyo kuwakumbusha Waislamu kuzitayarisha nafsi zao
kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambao umebakiza siku chache
kuingia ambapo Mwenyezi Mungu husogeza pepo kuwa karibu zaidi na waja
wake.
Katika
risala ya Waislamu wa msikiti huo, walisema zaidi ya Sh1.3 bilioni
zimetumika kwa ujenzi huo. Viongozi mbalimbali wa dini na Serikali
kutoka Zanzibar na bara walihudhuria wakiwamo Mufti Mkuu wa Zanzibar,
Sheikh Saleh Omar Kabi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji,
Sheikh wa Dar es Salaa, Alhadi Mussa na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan
‘Zungu’.
No comments:
Post a Comment