Mandla Mandela aendelea kulikoroga
WAKATI
mgogoro kati ya watoto wa Mandela na wajukuu ukizidi kutokota kuhusu
uhalali wa uchifu wa Mandla Mandela, yeye amejibu mapigo akisema Mfalme
Buyelekhaya Dalindyebo wa kabila la abaThembu ”hana akili timamu”.
Hiyo
inatokana na madai yaliyotolewa na mfalme huyo kwamba Mandla hakuwa
chifu sahihi wa ukoo wa Madiba. Alidai kwamba hakukuwa na cheti chochote
halali kilichotiwa saini wakati mandla alipotawazwa kuwa chifu mwaka
2007 – sherehe ambazo zilisimamiwa na Mandela mwenyewe.
Gazeti
la Mail & Guardian wiki iliyopita liliripoti kuwa uchifu wa Mandla
ulilalamikiwa kabla ya Mandela kulazwa hospitalini, ikielezwa kama kweli
anafaa kuendelea kuwa chofu ikizingatiwa kuwa mama na baba yake
walimzaa bila kuoana.
Jumamosi
iliyopita, Dalindyebo alisema hawezi kumheshimu mtu “ambaye haheshimu
familia yake” na kusema Ndaba ambaye ni mdogo wake Mandla ndiye
anastahili kuwa chifu.
Lakini
juzi, Mandla alijibu mapigo kupitia kwa msemaji wake, Freddy Pilusa
akisema: “Tamko lililotolewa na Mfalme Dalindyebo kwamba amemuondolea
Mandla madaraka yake ya kimila ni kichekesho.
“Ni
mchakato mrefu wa kimila kumuondoa chifu. Huwezi kuamka tu asubuhi na
kuitisha mkutano wa wafuasi wako na kuchukua uamuzi mzito kama huo,”
alisema Pilusa.
No comments:
Post a Comment