HATIMAYE wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya Afrika kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..
Mabinti
hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya
zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza
na mwandishi wetu jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na
Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika
wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda
Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE) ambaye
alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana
hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa
mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado
wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.
Alisema
Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi
kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao
watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Jumapili
iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya
aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini
wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa
hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya
Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.
Wanawake
hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa
na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150
za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya
bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.
Baada
ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo
linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni
28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni
janga la kitaifa nchini.
Alisema
kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara
haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa
kujihusisha na dawa hizo.
Pia
alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za
Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na
kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti
magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
Pinda
alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya
katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.
Alisema
vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata
sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na
kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.
Melezo Kwa hisani ya Nipashe.
No comments:
Post a Comment