Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye |
Mabingwa
watetezi wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe
la Kagame), Yanga wataanza kutetea taji lao dhidi ya Express ya Uganda
katika mechi ya kundi C Juni 20 kwenye Uwanja wa Elfasher saa nane
mchana wakati Simba iliyopangwa kundi A la 'kifo' itashuka dimbani siku
inayofuata kuivaa El Mereikh.
Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo yatakayoanza Juni 18 hadi Julai 2 mwaka huu iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), timu nyingine zinazounda kundi C pamoja na Yanga ni Vital'O ya Burundi na Ports ya Djibouti wakati kundia la kundi A la Simba linahusisha pia timu za APR ya Rwanda na Elman ya Somalia.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa kundi B limezoa timu wenyeji zote tatu za Al Hilal, Al Nasri na Al Ahly Shandy pamoja na Tusker ya Kenya na Super Falcon kutoka Zanzibar.
Yanga ambao ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara watashuka tena dimbani Juni 22 mwaka huu kuikabili Ports na watakamilisha mechi za hatua ya makundi Juni 25 kwa kuvaana na Vital'O.