BARUA TOKA VODACOM
KAMANDA
wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amedai kuwa uchunguzi wa
awali kuhusu ujumbe unaodaiwa kutumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa
Mulongo, umetumwa na mtandao wa simu wa nje ya nchi.
Kamanda
alisema katika ujumbe huo ambao Lema anadai uliandikwa na Mkuu wa Mkoa
Mulongo na kutumwa kwenye simu yake Aprili mwaka huu, uchunguzi wa
polisi umeonyesha kwamba haukutumwa kupitia kampuni moja wapo ya simu za
mikononi ya hapa nchini.
“Katika
kipindi cha mwishoni mwa Aprili mwaka huu, vyombo vingi vya habari
vikiwemo radio, magazeti na mitandao ya kijamii viliandika na kutangaza
habari iliyoelezea shutuma zilizotolewa na Mbunge Lema kuwa aliandikiwa
ujumbe wa vitisho kwa njia ya simu na Mkuu wa Mkoa Mulongo na ulisomeka:
“Umeruka kihunzi cha kwanza nitakuonyesha mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi inayoitaka mimi.”
Kamanda
Sabas alisema ujumbe huo ulidaiwa kutumwa kutoka namba 0752960276
inayotumiwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo kwenda kwenye namba 0764150747
inayotumiwa na Lema. Alisema kufuatia tuhuma hizo, polisi walianza
uchunguzi kwa kuzingatia kuwa Mulongo alikanusha kutuma ujumbe wa aina
yo yote kwa Mh Lema.
Alisema
uchunguzi huo ulihusisha kampuni ya simu ambayo mtandao wake ulitumika
katika utumaji wa ujumbe husika. Alisema uchunguzi wa awali wa polisi
umebaini kuwa chanzo cha ujumbe huo mfupi hakikuwa kampuni ya simu
husika (hakuitaja) kwa vile ‘Centre Number’ iliyotumika kutuma ujumbe
huo mfupi wa maneno ni 44780200332, ambayo siyo ya mtandao wa kampuni
husika bali ni ya mtandao ulio nje ya nchi.
Alisema
uchunguzi zaidi unaendelea kubaini chanzo cha ujumbe huo mfupi wa simu
na mtu aliyehusika kutuma hatua za kisheria zitaweza kuchukua mkondo
wake.
No comments:
Post a Comment