Rais
wa Marekani Bw. Baraka Obama na Mkewe wanatarajia kufanya ziara ya
nchi tatu barani Afrika itakayojumuisha nchi za Senegal, Afrika ya
Kusini na Tanzania, Kuanzia tarehe 26 Juni hadi tarehe 3 Julai.
Katika
ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka
katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za
Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo
ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji
wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi
wa Kiafrika.
Rais
atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na
jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa
kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment