UONGOZI
wa Simba umechukua uamuzi wa kumpandisha kizimbani kiungo mshambuliaji,
Mrisho Ngassa kutokana na uamuzi wake wa kusaini mkataba wa miaka
miwili kuichezea Yanga.
Ngassa
aliyekuwa akiichezea Simba kwa mkopo kutoka Azam FC, amesaini mkataba
wa miaka miwili kuichezea Yanga lakini Simba wamesema walishasaini naye
mkataba wa mwaka mmoja.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa, Msimbazi wameamua
kufanya mambo yao kimya na wameamua kutumia mahakama ili iwe fundisho
kwa wachezaji wengine.
“Hakika
sasa tumeona suala hili si la kufanya kama filamu, maana wenzetu
(Yanga) pamoja na Ngassa wameamua kutufanyia uhuni. Wachezaji wanataka
kufanya Simba ni kama sehemu ya kuchota fedha na kuondoka.
“Kitu
kibaya zaidi tumegundua system (mfumo) ya soka imekuwa ikiwalinda sana
kutokana na ushabiki mkubwa uliopo katika kamati zilizo chini ya TFF.
Sasa sisi tumeona bora kuchukua hatua zaidi,” kilieleza chanzo cha
uhakika.
“Tutamfikisha
Ngassa mahakamani, tutadai zaidi ya Sh milioni 200 kama sehemu ya
kutaka fidia kutokana na mkataba tulioingia naye. Mkataba upo, msione
tumekaa kimya mnaona kama hatuna cha kusema.
“Ila
sasa tumeamua kufanya mambo kwa mfumo tofauti na leo (jana) usiku
tutakuwa na mkutano kwa ajili ya kujadili kuhusiana na suala hili na
tutajua lini rasmi apande kizimbani.”
Championi
Jumatano ndiyo lilikuwa la kwanza kuandika kuhusiana na Ngassa kusaini
Yanga miaka miwili na kueleza kila anachopata katika mkataba wake,
achana na wale waliosema katika stori yao eti anatarajia kusaini.
Kwa
mujibu wa chanzo hicho kutoka ndani ya Simba, mkataba kati ya Ngassa
ulipelekwa na kusajiliwa TFF tangu Desemba, mwaka jana.
Tayari
baba yake (soma Uk 2) amezungumzia kuhusiana na mwanaye kuhamahama na
Yanga imeshatangaza kumtambulisha kwa mashabiki Juni 3 (soma Uk 2).
Suala la Ngassa kutua Yanga limezua gumzo kubwa na huenda likazua mgogoro mkubwa baina ya timu hizo mbili.
Mwishoni
mwa mwaka jana, Ngassa alitua Simba kwa mkopo akitokea Azam, lakini
akakabidhiwa gari aina ya Toyota Verossa na Sh milioni 30 na Simba
kutangaza imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa
mkopo, lakini Ngassa mwenyewe amekuwa akisisitiza hana mkataba na
Msimbazi baada ya ule wa Azam kumalizika.
No comments:
Post a Comment