Na Salma
Said Zanzibar
KESI ya
jinai inayowakabili viongozi wa Dini wa Jumuiya ya Uwamsho na Mihadhara
imeanza kusomwa upya jana katika mahakama Kuu ya Zanzibar.
Kesi hiyo namba 9
ya mwaka 2012 ilisomwa mbele ya Jaji Fatma Hamid Mahmoud na Mwendesha
Mashtaka wa Serikali Bw. Ramadhan Nassib, ambae aliwataja washitakiwa
hao kuwa ni Farid Hadi (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52)
mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47)
mkaazi wa Makadara
na Azan Khalid (48) mkaazi wa Mfenesini mkoa wa Mjini wa Magharibi
Unguja.
Wengine ni Suleiman
Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi
wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, Ghalib
Ahmada Juma (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe na Abdallah Said (48) mkaazi wa
Misufini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Washitakiwa wote
kwa pamoja walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kuharibu mali, Uchochezi,
Ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la ttatu ni kula njama ya kufanya
kosa huku kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne Azan Khalid ambae
anadaiwa kufanya vitendo
vinavyoweza
kusababisha uvunjifu wa Amani.
Makosa yote hayo
yandaiawa kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 katika maeneo tofauti
ambapo washitakiwa hao walipotakiwa kujibu tuhuma zao walizikana.
Mara baada ya
kuwasomea mashtaka yao hayo Mwenesdha Mashtaka wa Serikali Bw. Nassib
alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo tayari umeshakamilika lakini hata
hivyo aliiomba mahakama hiyo kufanya subra ya kuweza kuamuwa maamuzi
yoyote kutokana na upande huo wa mashtaka kukata rufaa kitendo ambacho
alisema kwamba iwapo mahakama hiyo itaendelea na kesi hiyo kunaweza
mahakama ya rufaa ikatoa maamuzi ambayo yataweza kuathiri maamuzi ya
mahakama hiyo.
Kwa upande wa
mawakili wa watetezi uliokuwa ukiongozwa na Bw. Taufik Salum uliiomba
mahakama hiyo kuwapatia dhamana washitakiwa wake haohasa ikiangaliwa
kuwa tayari washitakiwa hao wameshakaa ndani kwa muda mrefu.
“Mhe Jaji
tumefurahi kuona kwamba kwa mara ya kwanza upande wa mashtaka unatamka
kuwa upelelezi umekamilika lakini isiwe sababu ya kuendelea kubakia
rumande wateja wetu kwa vile muda wa kukaa kwako umekuwa mwingi na
kupelekea haki yao ya msingi ya dhamana kunyimwa”,
alisema Bw. Salum.
Hata hivyo Jaji
Mahmoud alisema kuwa atayachukuwa maombi ya pande yote mbili na
kuyapitia kwa umakini ili baadae aweze kutoa maamuzi yaliyosahihi
kutokana na kuwa ni mgeni wa kesi hiyo na jalada lake amelipokea kwa
muda mchache ambao haukpata nafasi ya kuipitia.
“Nayachukuwa maombi
yote mawili nitayatafakari kwa kina na kuja kutoa maamuzi unaofaa”,
alisema.
Hata hivyo Jaji
huyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 27 mwaka huu.