Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani
(The World Intellectual Property Organization –WIPO) Dr. Francis Gurry
(wa tatu kushoto) akiwa na ujumbe wake wakati alipomtembelea Ikulu
jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani (The World Intellectual Property
Organization –WIPO) Dr. Francis Gurry katika mazungumzo na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alipomtembelea
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda (wa kwanza kushoto) na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi.Joyce Mapunjo (katikati)
wakimsikiliza kwa makini Rais Dr. Kikwete wakati akizungumza na
Mkurugenzi Mkuu wa WIPO (hawapo pichani).
Baadhi ya Maafisa mbalimbali wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mh.
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry aliyeambatana na Ujumbe wake. Wa pili
kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda.
Rais
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimwonyesha Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr.
Francis Gurry mmoja ya mti wa Mwembe (haupo pichani) uliodumu kwa miaka
mingi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa
WIPO Dr. Francis Gurry mara baada ya mazungumzo alipomtembelea Ikulu
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr.
Abdallah Kigoda.
Rais Dr. Jayaka Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).