MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa watumiaji
vibaya na wahalifu wote wa mitandao nchini, kuwa siku zao zinahesabika
kwani ifikapo Septemba mosi, mwaka huu, Sheria ya Uhalifu wa Mitandao
itaanza kutumika na wengi huenda wakaishia gerezani.
Mamlaka hiyo imebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inaongoza kwa kuwa na
watumiaji vibaya wengi wa mitandao ya kijamii, jambo linalosababisha
taarifa za mitandao mingi kutoaminika hadi nchi za nje kutokana na kujaa
uzushi, uongo, uchochezi na lugha na picha za matusi.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa
TCRA, Innocent Mungy alikiri kuwa pamoja na kwamba mamlaka hiyo imefanya
kazi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya utumiaji sahihi wa mitandao hiyo,
bado matumizi yake si mazuri hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na
kwa watu maarufu.
“Napenda kuwatahadharisha Watanzania na watumiaji wa mitandao hii kwa
ujumla kuwa sheria hii si ya kupuuzwa, kwani kwa hali ilivyo wengi
watatozwa faini na watashindwa kulipa na kuishia gerezani,” alisisitiza. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Alisema kutokana na kukithiri kwa matumizi mabaya ya mitandao nchini,
kwa sasa nchi nyingi haziamini tena taarifa za mitandao ya kijamii na
wala hawazitumii hali inayopaswa kubadilishwa.
“TCRA tumebaini kuwa watu wengi wanatumia mitandao hii lakini hawajui
hasa matumizi yake sahihi, tunashauri kabla mtu hajafungua mtandao wake
kama vile blogu, ukurasa wa facebook au hata whatsApp lazima
wajielimishe kwanza kuwa wanafungua kwa malengo gani, na wataitumiaji
kwa manufaa yao na si vinginevyo,” alisisitiza Mungy.
Alisema mamlaka hiyo kazi yake kubwa ni kusimamia matumizi ya
mitandao hivyo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, itahakikisha
inadhibiti kwa kuelimisha na kuwabaini wale wote wanaotumia vibaya
mitandao hiyo.
“Kazi yetu sisi si kuwakamata hawa wahalifu, sisi tunasimamia na tuna
uwezo wa kuwatambua wale wote wanaotumia vibaya mitandao hii hata kama
watabadilisha kadi zao za simu mara 300 na kubadili majina, tuna uwezo
wa kuwatambua na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria pale tunapotakiwa
kwa mujibu wa taratibu,” alisisitiza. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Alisema tayari wameshaanza kampeni ya kuelimisha matumizi sahihi ya
mitandao kupitia vipindi na semina zinazojumuisha kada mbalimbali muhimu
kama vile wasanii na vyombo vya habari juu ya kujihadhari na matumizi
mabaya ya mitandao.
“Hivi karibuni tulifanya semina ya wasanii ambao ndio waathirika
wakubwa wa matumizi haya ya mitandao na kuwaelimisha namna ya kuitumia
mitandao hii, pia vyombo vya habari tumevielimisha na kuvisisitiza
kutotegemea taarifa za mitandao hasa kipindi hiki cha uchaguzi kwa kuwa
nyingi si sahihi,” alisema bosi huyo wa TCRA.
Tayari Rais Jakaya Kikwete ameshasaini Sheria hiyo ya Makosa ya
Mtandao ya Mwaka 2015 na inatarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi Septemba
mosi, mwaka huu. Sheria hiyo katika eneo la adhabu kwa wahalifu wa
mtandao pamoja na wasambazaji wa picha za utupu na ngono, wasambazaji wa
taarifa za uongo, za kibaguzi na matusi na watu wengine wanaofanya
udanganyifu unaohusu kompyuta, adhabu ni kwenda jela hadi miaka 10 au
kulipa faini isiyopungua Sh milioni 50.
Kwa upande wa kusambaza picha za ngono, matusi, uasherati atalipa
faini isiyopungua Sh milioni 30 au kwenda jela miaka 10 au vyote. Lakini
mtu atakayesambaza picha za utupu atalipa faini isiyopungua Sh milioni
20 au kwenda jela miaka saba au kutumikia adhabu zote kwa pamoja. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Pia kwenye muswada huo mtu ambaye atatoa taarifa, takwimu au maelezo
kwa njia ya picha, maandishi, alama au aina nyingine yoyote zikiwa ni za
uongo akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua Sh milioni tatu au
kutumikia kifungo jela kisichopungua miezi sita au vyote.
Kwa upande wao, Jeshi la Polisi Tanzania, limesema tayari limeanza
kuchukua hatua dhidi ya watumiaji vibaya wa mitandao ya kijamii na hadi
sasa imekamata watumiaji hao wengi na wako katika hatua ya kuhojiwa na
wengine kufikishwa mahakamani.
“Natumia fursa hii kuwaonya watu waache tabia ya kutengeneza ujumbe
wa uchochezi, matusi, uongo na uzushi kwa visingizio vya itikadi, dini
na siasa kwani Jeshi la Polisi halitovumilia tabia hizo na
watakaobainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema msemaji
wa jeshi hilo, Advera Bulimba.
Alikiri kuwapo na tabia ya watu kuandika kwenye mitandao ya kijamii
taarifa za uchochezi na uzushi dhidi ya watu maarufu wakiwemo viongozi
au taasisi na baadhi yao wanachunguzwa na wakibainika watachukuliwa
hatua za kisheria.
Alitolea mfano wa mmoja wa watumiaji mtandao ambao jeshi hilo
lilibaini aliandika taarifa za uchochezi kuhusu tukio la ujambazi na
mauaji la Kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam na sasa
anakabiliwa na kesi ya uchochezi mahakamani. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment