Mshambuliaji wa zamani wa klabu
za Manchester United, Atletico Madrid, Intermilan Diego Forlan jana
ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Uruguay baada ya
kuichezea timu hiyo tangu mwaka 2002.
Forlan,35, ambaye kwa sasa
anakipiga katika klabu ya Cerezo Osaka ya nchini Japan amekuwa msaada
mkubwa kwa timu ya taifa ya Uruguay na mwaka 2010 aliiwezesha timu hiyo
kushinda nafasi ya 3 kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika huko
nchini Afrika kusini huku yeye akibeba tuzo ya mchezaji bora wa
mashindano hayo baada kuonesha kiwango bora.
“Ninawashukuru kwa wote walionipa
ushirikiano tangu naanza kuichezea timu ya taifa mwaka 2002, ninaamini
timu itaendelea kufanya vizuri na nimechukua uamuzi huu ili kutoa kwa
nafasi kwa wachezaji wengine ambao ninatumaini wataisadia timu hii”
alisema Forlan.
Mchezaji huyo aliyepata sifa
nyingi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu mpaka
anatangaza kustaafu tayari ameshaichezea timu ya taifa ya Uruguay
michezo 112 na kufunga magoli 36. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment