Mh. Mboni Mhita akizungumza na moja wa majeruhi katika hospitali ya wilaya ya Mufindi
Mkuu wa wilaya akiwa na wana kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo eneo la tukio
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Mkuu wa wilaya akichunguza kontena lililohusika katika ajali hiyo
Mkuu wa wilaya akipewa maelekezo ya kiutaalamu kutoka kwa mmoja ya wana kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo
Wana kamati wakijadilina jambo kuhusiana na ajali
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mh. Mboni Mhita akitoa ufafanuzi wa jambo fulani.
Mkuu
wa wilaya ya Mufindi akiangalia namna ambavyo basi limeharibika vibaya
baada ya ajali na kutilia shaka ubora wa bodi ya gari hiyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kamati ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ikidadisi baadhi ya vitu katika ajali hiyo
Mkuu wa wilaya akidadisi vitu vilivyopo eneo la tukio. |
Katika kuhakikisha wananchi wanapewa taarifa sahihi
kuhusiana na chanzo cha ajari ya gari la abiria na lori iliyotokea tarehe Marchi 11, mwaka huu, maeneo ya Changarawe wilayani Mufindi, Mkuu wa wilaya hiyo Mboni
Mhita ameunda kamati maalumu ya kuchunguza chanzo cha ajali hiyo ambayo
imepoteza maisha ya zaidi ya watanzania
arobaini
Kamati hiyo ambayo imeundwa na timu ya wataalamu mbalimbali wakiwamo madaktari, maafisa wa TAKUKURU, mafundi wa magari, wakuu wa majeshi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Timu hiyo ya uchunguzi imeanza kazi masaa kumi na mbili baada ya ajali kutokea, ambapo kamati hiyo ili kujiridhisha zaidi ilitembelea tena eneo la ajari na kufanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini sababu mbalimbali.
Aidha Mkuu wa wilaya hiyo amewataka wananchi kuwa wavumilivu kwani timu hiyo ya wataalamu itatoa ripoti iliyokamilika hivi karibuni.

Wakati huohuo mkuu wa wilaya huyo anaishukuru kamati ya
uangalizi wa mali za marehemu pamoja na majeruhi kwa kushirikiana vizuri
kuhakikisha eneo la ajali kunakuwa na usalama na huduma za haraka kwa
waathirika wa ajali hiyo kamati hiyo ilijumuisha viongozi wa dini na wananchi
wa eneo ambalo ajali ilitokea.
Pia ametoa salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu pamoja na kuwatembelea majeruhi walionusurika katika ajali hiyo.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Pia ametoa salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu pamoja na kuwatembelea majeruhi walionusurika katika ajali hiyo.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
ENDELEA KUTEMBELEA MTANDAO HUU PUNDE TUTAKUPA RIPOTI KAMILI YA KAMATI HIYO
Habari Na Kayanda Manyanya
Habari Na Kayanda Manyanya
No comments:
Post a Comment