Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua
ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata,Wilayani
Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali
itajenga nyumba 403 ambazo zimebomolewa na mvua kubwa iliyonyesha wiki
iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu
649 kukosa mahali pa kuishi.
Kauli hiyo aliitoa jana kwenye kijiji cha Mwakata
baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na mvua hiyo na kujionea maisha
duni wanayoishi watu hao.
Akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wake
Rais Kikwete alisema Serikali iko pamoja na wananchi hao na
itahakikisha makazi yao yanarejea katika hali yake ya kawaida kwa
kuwajengea nyumba hizo.
Pia,
Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Kujenga
Taifa(JKT) wajenge nyumba hizo bila kupitia mkandarasi yeyote kama vile
ulivyo ujenzi wa Serikali kwa kuwa ujenzi wa jeshi unaisha kwa muda
mfupi na hakuna uchakachuaji. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu
zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click
Neno Jambo Tz.
Aliwataka viongozi mkoani Shinyanga kuhakikisha
ujenzi huo hautangazwi na kuagiza JKT kwenda kwenye eneo hilo kufanya
tathmini ya ujenzi huo ili uanze mara moja.
Rais Kikwete aliwatoa wasiwasi wananchi wa Mwakata
waliokumbwa na tatizo hilo kwamba Serikali itahakikisha wote wamepata
chakula hadi mwisho watakapolima na kupata mavuno na tukio hilo
wasilihusishe na imani za kishirikina.
Alisema mvua hizo ni za kawaida ambazo hutokana na
mabadiliko ya tabia ya nchi na si ushirikina hivyo aliwataka wananchi
hao waendelee kuwa na hisia hizo lakini wasilichukulie kwa uzito swala
la ushirikina wakatafuta mchawi wa mvua hiyo
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga
alimwambia Rais Kikwete kwamba mvua hiyo licha ya kuua watu 47 pia
imeharibu mazao hekari 2,332 pamoja na visima 53 vya maji ya kunywa.
Rufunga alisema mpaka kufikia sasa wahisani
mbalimbali wamechangia kwenye tukio hilo Sh64 milioni pamoja na tani 63
za unga wa sembe pamoja na mahitaji mbalimbali ya kibinadamu yakiwamo
mabati zaidi ya 1,000
Kufuatia
hali hiyo Rais Kikwete alisema Serikali
itatumia zaidi ya Sh 2 bilioni kurejesha makazi hayo huku akitupilia
mbali madai ya Mbunge wa jimbo la Msalala, Ezekiel Maige ya kuitaka
Serikali ifute ushuru wa vifaa vya ujenzi ili wananchi wanunue kwa bei
rahisi wajenge nyumba za kisasa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei
nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/
Click Neno Jambo Tz.
Na Mwanachi
Na Mwanachi
No comments:
Post a Comment