Viongozi
wa wanafunzi huko Hong Kong wamekubali kukutana na upande wa serikali
kujadili malalamiko yao siku tano baada ya maandamano makubwa ya
kupigania demokrasia.
Hiyo inafuatia mwaliko kutoka kwa mkuu wa
utawala wa Hong Kong CY Leung. Alitoa taarifa hiyo muda mfupi kabla ya
kumalizika kwa muda wa mwisho uliowekwa na wanafunzi hao waliotishia
kuvamia majengo ya serikali iwapo mkuu huyo hatajiuzulu.Muda wa mwisho uliowekwa na wanafunzi hao umemalizika salama.
Bwana Leung amesema atabakia madarakani na kuwaonya waandamanaji kuwa watapata matatizo iwapo watavamia majengo ya serikali.
Kumekuwa na makabiliano makali katika eneo la majengo ya serikali ambapo waandamanaji wamekuwa wakiendelea kudai uchaguzi wa haki mwaka 2017. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment