Dar es Salaam/Mwanza. Rais Jakaya Kikwete
ameshauriwa kunusuru mchakato wa kupata Katiba Mpya ili usisimame kwa
kuvua koti la Uenyekiti wa CCM na kubaki na Urais ili awaeleze wananchi
nini cha kufanya kupata Katiba Mpya.
Ushauri huo umetolewa na viongozi mbalimbali wa
vyama vya siasa na wasomi walioshiriki katika mdahalo wa Katiba
uliofanyika jijini Dar es Salaam na Mwanza jana. Walisema kuwa Rais ana
wajibu kuunusuru mchakato huo kwa kuwa yeye ndiye aliyeuvuruga kwa
hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge Maalumu la Katiba iliyoonekana kuelemea
upande wa chama chake CCM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete amekuwa
kigeugeu juu ya Muundo wa Serikali za Muungano kama zilizopendekezwa
kwenye Rasimu ya Kwanza na ya Pili ya Katiba.
Alisema kuwa Rais Kikwete alionyesha wazi
kukubaliana na Muundo wa Serikali tatu, kwani kabla Rasimu ya Pili ya
Katiba haijapelekwa kwenye Bunge Malaumu la Katiba ili kujadiliwa,
alisaini kuonyesha kuwa amekubaliana na yaliyopendekezwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
cha Mwanza (Saut) Dk Slaa alisema:
“Rais Jakaya Kikwete amekuwa kigeugeu, kwani yeye
ndiye aliyesaini Rasimu ya Pli ya Katiba ili ikajadiliwe kwenye Bunge
Maalumu la Katiba.” Aliongeza: “Kwa kuwa ndiye mtu wa mwisho kuruhusu
rasimu hiyo ijadiliwe kwenye Bunge Malaamu la Katiba ni wazi
alikubaliana na kilichopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
iliyopendekeza Muundo wa Serikali Tatu, hivyo inashangaza kuona leo
anageuka na kutaka Serikali mbili.”
Dk Slaa ambaye pia ni kiongozi katika Umoja wa
Katiba ya Wananchi Nje ya Bunge (Ukawa), alisema kuwa katika mikoa 17
waliyozunguka na kufanya mikutano na wananchi, wamebaini kuwa Rasimu ya
Katiba ya Pili wananchi hawaifahamu na kwamba hiyo ni njia ya CCM
kuchakachua maoni yao yaliyomo kwenye rasimu hiyo, wakati wa kupiga kura
za maoni.
Alisema wanatambua ujanja unaofanywa na CCM kutaka
kupitisha mambo wanayoyataka wao, lakini wao watendelea kuwaelimisha
wananchi ili watambue kwamba maoni yao ndiyo nguzo ya kuwapa Katiba bora
na siyo vinginevyo.
“Tumefanya mikutoano mikoa 17, lakini kote
tulipopita wananchi wametuambia hawaifahamu Rasimu ya Pili ya Katiba
kutokana na janja ya CCM kuficha rasimu ya hiyo ili wananchi
wasiifahamu. Kutokana na hilo ni wazi kwamba wanataka kuchakachua maoni
ya wananchi kwenye kura za maoni,”alisema Dk Slaa.
Akinukuu maneno kutoka katika hotuba ya Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa mwaka 1995 Dk Slaa alisema:
“Watu wapumbavu ni wale wanaoamini kwamba Katiba haibadiliki.”
Alisema lazima Katiba ibadilike na kwamba wananchi
ndiyo wenye Katiba, hivyo siyo busara kutaka kuchakachua maoni yao na
kuweka maoni ya chama au mtu binafsi.
“Watu wanamini kuwa Katiba haiwezi kubadilika, mimi naona ni upumbavu, kwani hata Mwalimu Nyerera aliwahi kusema hivyo kwenye hotuba yake ya mwaka 1995,” alisema Dk Slaa.
“Watu wanamini kuwa Katiba haiwezi kubadilika, mimi naona ni upumbavu, kwani hata Mwalimu Nyerera aliwahi kusema hivyo kwenye hotuba yake ya mwaka 1995,” alisema Dk Slaa.
Tundu Lissu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu
alisema kuwa kuna mambo mema ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifanya na
mengine ambayo siyo mema, hivyo Watanzania na wasomi wanapaswa
kuyachuja na kuyakataa mabaya na kuchukua mema.
Alisema katika mambo mabaya ambayo Mwalimu Nyerere
aliacha ni pamoja na kuwarithisha Watanzania hofu, jambo alilosema hadi
sasa limewatawala.
“Nyie kama wasomi wa Saut naomba niwaambie kwamba
katika mambo mabaya ambayo Mwalimu Nyerere aliwarithisha Watanzania ni
hofu, jambo ambalo hadi leo linaawatawala kwani Watanzania wengi
wanaogopa kusema kwa kuhofu kufukuzwa kazi au vyuo, “alisema Lissu na
kuongeza:
“Mmoja ya mfumo mbaya ambao Mwalimu Nyerere
aliuanzisha baada ya kupata uhuru mwaka 1962 ni kuwaweka watu kizuizini.
Hii ilikuwa inatokea kwamba unakamatwa na watu usiowajua na unawekwa
kizuizini, ”alisema.
Kutoka Dar es Salaam, Muungano wa Asasi za Kiraia
(AZAKI), umemtaka Rais Jakaya Kikwete kunusuru mchakato wa kupata Katiba
Mpya usisimame ukieleza kuwa yeye ndiye aliyeuvuruga.
Akizungumza katika mkutano wa AZAKI, jijini humo
aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga
Baregu, alisema kuwa mchakato mzima ulikwenda vizuri, lakini baada ya
Kikwete kulihutubia Bunge Maalumu la Katiba, mwelekeo wa Bunge hilo
ulibadilika.
Alisema kuwa Rais Kikwete alikwenda kulihutubia
Bunge kama kiongozi wa CCM, badala ya kiongozi wa nchi, ambapo aliweka
msimamo wa chama chake wa kutaka Muundo wa Serikali mbili. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
“Rais apate ujasiri akiwa kama kiongozi wa nchi na
siyo kama kiongozi wa CCM, awahutubie wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba na kuwataka wajadili Katiba ya wananchi na siyo ya chama wala
yake binafsi,” alisema Baregu.
Aliongeza kuwa kama Rais hatalinusuru Bunge hilo
na kila mtu akafanya anavyotaka au kwa masilahi ya chama chake kama
ambavyo ameonyesha mfano, demokrasia nchini haitawezekana.
Baregu aliwataka wajumbe watumie miezi miwili
iliyobaki kujipanga upya iwapo wana nia ya dhati ya kuendelea na
mchakato huo, ili ipatikane Katiba bora ya wananchi akionya kwamba,
tofauti na hapo Watanzania hawatakubali.
Kauli ya Baregu pia iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Chama cha
Sheria Zanzibar, Awadhi Ally Saidi ambaye ni pia ni miongoni mwa
waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, aliyesema kuwa inafaa
Rais awahutubie wajumbe na kuwakumbusha kuwa jukumu lao ni kujadili
Rasimu ya Katiba ya kuipitisha na siyo kuondoa vipengele.
“Ndiyo maana walipewa siku 70 kujadili Rasimu ya
Katiba, lakini walitumia siku 21 kutunga kanuni ambazo zilitungwa na
Baraza la Wawakilishi likishirikiana na Bunge la Muungano,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment