Wakati mamilioni ya fedha za
Watanzania yakipotea kila mwaka kutokana na ufisadi na misamaha ya kodi,
imebainika kuwa baadhi ya magereza nchini hayafai kutumiwa na wafungwa
kutokana na kukosa sifa ukiwemo uchakavu wa majengo.
Ripoti ya utafiti uliofanywa na Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora kwenye magereza na vituo vya polisi 102 katika
mikoa 12, inaeleza kuwa magereza 12 hayafai kutumiwa na binadamu.
Hali hiyo inaamanisha kwamba magereza hayo siyo tu
ni hatari kwa wafungwa na mahabusu, bali pia kiwa watumishi wa Idara ya
Magereza. Ripoti hiyo inaweka bayana kuwa magereza hayo yana hali mbaya
kutokana na majengo yake kujengwa miaka mingi iliyopita, huku mengine
yakikabiliwa na ukosefu wa mwanga wa kutosha.
Magereza yaliyotajwa kukosa sifa za kutumiwa na
binadamu ni Rombo, Nzega, Geita, Ngudu, Kasungamile, Ukerewe, Mugumu,
Musoma, Bunda, Ushora, Mang’ola na Bariadi.
“Hali kwenye haya magereza ni kinyume na Kanuni
namba 10 ya Umoja wa Mataifa, inayozungumzia namna ya kuwahifadhi
wafungwa ambayo inataka sehemu za kulala zikidhi vigezo vya kiafya, hali
ya hewa, nafasi ya kutosha, joto na mwanga wa kutosha,” inasema sehemu
ya ripoti hiyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Utafiti huo uliokuwa ukiangalia hali za watoto
magerezani kwa mwaka 2012/2013 unaeleza kuwa maboresho ya majengo ya
magereza yaliyochakaa ni jambo ninalohitaji kupewa kipaumbele katika
mpango endelevu wa kuboresha magereza nchini.
Hata hivyo, taarifa hiyo imeyamwagia sifa magereza
ya Igunga, Kahama, Arusha, Karanga, Handeni, Singida, Kiomboi,
Shinyanga, Uyui na Butimba kuwa yanapitisha mwanga na hewa ya kutosha
kwa wafungwa na mahabusu. Imebainisha namna wafungwa watoto walivyokuwa
wakipigwa, kutishwa na kuzuiwa kutembelewa na ndugu zao kama sehemu ya
adhabu.
Asilimia 55 ya watoto waliohojiwa walisema
walipewa adhabu mbalimbali, ambapo magereza yaliyoyajwa kutekeleza
vitendo hivyo ni Mugumu, Sengerema, Butimba, Lushoto, Tanga, Karanga,
Tukuyu, Ngudu na Rombo. Kuhusu utolewaji wa elimu ndani ya magereza,
ripoti hiyo inabainisha kuwa asilimia 51.6 ya watumishi wa magereza
waliohojiwa walisema hakuna programu yoyote ya elimu.
“Kanuni namba 38 ya Umoja wa Mataifa inayohusu
ulinzi wa watoto inasema kuwa, kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule
anatakiwa kuwa kwenye darasa la umri wake,” inasema.
Mchambuzi wa Sera wa Shirika la Haki Elimu,
Boniventura Godfrey akizungumzia ripoti hiyo alisema Katiba inatoa haki
ya elimu kwa mtoto kuwa ni lazima na siyo hiari.
“Mtoto anatakiwa apate elimu, hata akiwa gerezani kwa sababu kosa alilolifanya halina uhusiano na kupata elimu,” alisema.
Mkazi wa Mtoni Kijichi, wilayani Temeke, Rehema
Kyaruzi alipohojiwa kuhusu ripoti hiyo, alisema Serikali inapaswa
kuwaruhusu watoto wanaofanya makosa madogo kutumikia adhabu zao
nyumbani. Alisema anaamini iwapo watoto hawatapewa nafasi ya kushiriki
kwenye masomo au michezo wanaweza kuathirika kisaikolojia na kiafya. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
“Hakuna mzazi hata mmoja anaweza kutamani mtoto wake apelekwe gerezani.Hilo jambo linaumiza sana, lakini ikitokea, hakuna namna zaidi ya kulipokea bila kulikubali,” alisema.
Na Mwananchi
“Hakuna mzazi hata mmoja anaweza kutamani mtoto wake apelekwe gerezani.Hilo jambo linaumiza sana, lakini ikitokea, hakuna namna zaidi ya kulipokea bila kulikubali,” alisema.
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment