Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwamo la mwanamke mmoja kudaiwa kuuawa na mume wake kutokana na wivu wa mapenzi.
Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwamo la mwanamke mmoja kudaiwa kuuawa na mume wake kutokana na wivu wa mapenzi.
Katika tukio la kwanza, Mkazi wa Kijiji cha
Liwalanje, wilayani Mbozi, Christina Hayola (35) amefariki dunia baada
ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kifuani na miguuni na mtu anayedaiwa
kuwa mume wake.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi
alisema uchunguzi wa awali umebaini kwamba chanzo cha mauaji ni wivu wa
mapenzi na kwamba polisi wanamsaka mhusika.
Katika tukio la pili, Msangi alisema mkazi wa
Isanga jijini hapa, Abdi Sanga aliuawa kwa vipigo baada ya kutuhumiwa
kuwa wizi katika eneo la Forest.
Alisema marehemu anadaiwa alikuwa na mwenzake ambaye alitoroka baada ya kuiba vitenge vyenye thamani ya Sh70,000.
Katika tukio la tatu na la nne, alisema mwanafunzi
wa Shule ya Msingi Ibumila wilayani Mbarali, Fitina Mwandosya alifariki
dunia baada ya kudondoka kutoka kwenye trekta dogo aina ya
‘Powertiller’ alilokuwa amepanda akitoka kuvuna mpunga.
Alisema mwanafunzi huyo alipatwa na mkasa huo juzi wakati wanarudi na wenzake waliokwenda kuvuna mpunga wa shule.
Wakati huohuo mwanafunzi mwingine wa kidato cha
pili Sekondari ya Makongorosi, wilayani Chunya, Aden Ngombe(17)
amefariki dunia juzi baada ya kugongwa na lori aina ya scania alipokuwa
akikatisha barabara.
Msangi alisema polisi walimkamata dereva wa lori na kubainika alikuwa amelewa pombe.
Katika matukio mengine watu wanne wanashikiliwa na
polisi kwa tuhuma mbalimbali zikiwamo za kukutwa na bastola kinyume na
sheria.
Kamanda wa polisi alisema aliyekamatwa na bastola
ni mkazi wa Kijiji cha Itentula, Mbozi aliyekuwa na bastola aina ya
Baby. risasi tatu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment