Wadau wengi wa michezo wanakua wakiwaangalia sana wachezaji
waliotoka Bongo kwenda nje ya nchi kucheza soka la kulipwa na miongoni
mwao ni Mbwana Samatta ambaye kwa mshahara wake peke yake umezua gumzo
mtaani,
Sasa taarifa kutoka TFF ambayo ame-amplify Ofisa habari wa TFF
Boniface Wambura unaambiwa Wachezaji watatu kutoka Tanzania ambao ni
wachezaji wa mpira wa miguu tayari wameombewa hati ya uhamisho wa
Kimataifa[ITC] ili wakacheze katika nchi za Thailand na Ujerumani.
Miongoni mwao ni mchezaji Khamis Mroki Jamal ambaye timu yake ilikua
Daraja la Kwanza ya Polisi Dar es Salaam yeye ameombewa ITC na Chama cha
Mpira wa Miguu Thailand (FAT) ili akajiunge na Kabinburi ya nchini
humo.
Wengine ni Said Ali Nassor aliyekuwa akichezea FC Turkey ya Zanzibar
na Samuel Chuonyo hao wote wameombewa na ITC na Chama cha Mpira wa Miguu
Ujerumani (DFB) kwa ajili ya kujiunga na klabu ya VfB Eichstatt.
Kwa sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi
maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika ikiwemo ridhaa ya
klabu zao za hapa Tanzania TFF itatoa ITC hizo na jamaa kwenda kujiunga
na timu hizo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment