Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba.PICHA|MAKTABA
Dar es Salaam. Kituo cha Taarifa kwa
Wananchi (TCIB), kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kubadilisha
mfumo wa uendeshaji Uchaguzi Mkuu ikiwamo kuweka kipengele
kitakachowalazimisha wagombea wa nafasi za uongozi kupima afya zao ili
kuepuka kuchaguliwa viongozi wenye maradhi yatakayowafanya washindwe
kumudu majukumu yao ya kazi.
Pia kimeitaka NEC kuweka zuio la
kufanyika kwa uchaguzi na kutoza faini kali kwa mgombea anapotangaza
kujitoa katika hatua za mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi wenyewe.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi
Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba wakati akitoa tathimini ya uchaguzi mdogo
wa udiwani uliofanyika katika Kata 27 na funzo kuelekea uchaguzi wa
Serikali za Mitaa na ule wa Ubunge katika Jimbo la Kalenga mwezi ujao.
Alisema, Novemba 2012 kulifanyika
uchaguzi kujaza nafasi 29 za udiwani wakati Juni 2013 kulifanyika tena
uchaguzi katika kata 22 na mwezi huu umefanyika uchaguzi katika kata 27,
huku baadhi ya kata zikiwa tayari zimekwisharudia chaguzi zaidi ya mara
moja ndani ya kipindi cha miaka mitatu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
"Tangu mwaka 2010 ulipofanyika
uchaguzi mkuu, kumefanyika chaguzi tatu za madiwani nafasi hizo kuwa
wazi zilitokana na vifo hivyo kuna haja ya viongozi wetu kuwapima afya
zao hata magonjwa ya kisasa ili kuepusha kufanya chaguzi za mara kwa
mara zenye gharama kubwa fedha zinazoweza kusaidia katika miradi mingine
ya maendeleo," alisema Kibamba.
Aliongeza: "Unakuta mtu anachaguliwa
na anapewa nafasi nyeti serikalini lakini afya yake hairidhishi na
mwisho wa siku anafariki yote haya ni kutokuwapima afya zao."
Kibamba akizungumzia hatua ya kuchukua
na kurejesha fomu alisema kulitokea dosari kadhaa, ambazo zimekuwa
zikijirudia mara kwa mara mfano, mgombea kushindwa kurejesha fomu kwa
wakati katika Kata ya Nduli mkaoni Iringa na kutekwa kwa mgombea katika
kata ya Mtae mkoani Tanga wakati akirejesha fomu.
Alisema matukio kama hayo yanatakiwa
kuangaliwa kwa jicho la tatu na NEC kuzuia kufanyika kwa uchaguzi ili
kutoa nafasi kwa walioshindwa kuwasilisha fomu kutafutiwa ufumbuzi.
"Hapa kuna dalili za rushwa, mtu
huwezi kuomba kugombea harafu ukajitoa hatua za mwisho, hivyo NEC iweke
adhabu kali kwa watakaokuwa wakijitoa na wanaovamiwa," alisema Kibamba
Akizungumzia kauli tata ya Rais Jakaya
Kikwete aliyoitoa katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mjini
Dodoma mwishoni mwa wiki kuwa unyonge kwa wanachama wake sasa basi na
ile ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoitoa Bungeni mwaka jana ya
kuwapiga wanaokaidi amari ya vyombo vya dola alisema ni kauli za
kichochezi zinazotakiwa kutafutiwa ufumbuzi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
chanzo MWANANCHI
No comments:
Post a Comment