Na DANIEL MBEGA
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea
kutimua vumbi katika harakati za kutafuta bingwa katika mwaka wake wa 49
tangu harakati za kutafuta klabu bingwa zilipoanza mwaka 1965.
Mikiki mikiki yote hii isingekuwepo leo kama lisingekuwa wazo la kocha
wa Taifa Stars wa wakati huo, Milan
Celebic wa Yugoslavia, alilolitoa mwaka 1964 kama njia ya kusaidia
kuchagua wachezaji wa timu ya taifa badala ya kutegemea michuano ya
Sunlight Cup (sasa Taifa Cup).
Badala ya michuano ya Sunlight
iliyohusisha klabu na timu za Majimbo, Celebic aliona kulikuwa na
umuhimu wa kuwepo mashindano ya klabu pekee katika ngazi ya taifa na
siyo yale ya mkoa, hasa wa Pwani (Dar es Salaam ya sasa), hivyo
'akaliuza' wazo lake kwa Chama cha Ligi ya Soka cha Dar es Salaam (DFLA)
ambao walianzisha mashindano hayo mwaka 1965 yakijulikana kama Ligi ya
Taifa.
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TFA (TFF)
uliofanyika kati ya Desemba 19-20, 1964 (Jumamosi na Jumapili) katika
Ukumbi wa Arnautoglou mjini Dar es Salaam ndio uliojadili pamoja na
mambo mengine, uanzishwaji wa Ligi ya Taifa. Tembelea jambotz8.blogspot.com na kenypino.blogspot.com kila siku.
No comments:
Post a Comment