INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili
mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo
wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.
Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi
jijini Dar es Salaam ameingia katika dimbwi la AIBU baada ya kunaswa
akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.
Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti
huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili)
katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye
alikuwa safarini.
Kikao
cha dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi wetu kutoa maelekezo juu
ya habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za jiji la Dar usafiri
uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.
Haraka
timu ya waandishi wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya
walikwama.
Taarifa
iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla
timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya
kumuondoa denti huyo.
Wikiendi iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu
kilekile kilipiga tena simu kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa
kwa mara nyingine amemwingiza yule denti chumbani kwake.
Timu
A iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo la tukio na kuliweka
chini ya uangalizi huku timu B ikielekea katika Kituo cha Polisi cha
Wailesi na kuomba ushirikiano wao.
Timu
ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na
waandishi wetu kwenda eneo la tukio.
Waandishi
wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba
hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama
walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa
darasani.
Binti huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya
kukutwa chumbani hapo, alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki
kwa muda mrefu baada ya kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.
“Ni
kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa. Nyumbani kwetu ni
Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni lakini Taliki
aliniambia nije kwake.
“Naombeni
mnisamehe jamani. Mama akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na
ninaahidi mbele yenu kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba
(Taliki),” alisema denti huyo.
Denti
huyo alitoa namba ya simu ya mama yake mzazi ambapo alipigiwa na kufika
eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto wake anavyoharibiwa wakati yeye
akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea maisha.
Mama
wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda
wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.
UPUUZI
WA TALIKI
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye
muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu
alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).
“Ndugu
zangu wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma
(utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa
anamtengenezea yule binti wa watu maisha?).”
Utetezi
wake haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi
Wailesi na kufunguliwa mashitaka katika Jalada nambaWS/RB/585/2013 –
KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.
GPL
No comments:
Post a Comment