Dar es Salaam. Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania, JWTZ, limekanusha taarifa zilizotapakaa kwenye
mitandao kuwa askari wa jeshi hilo waliokwenda huko kwa ajili ya kulinda
amani,wameanza kujihusisha na makahaba.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Mtandao wa
www.congodrcnews.com wanajeshi wa Tanzania wameanza kujihusisha na
ubakaji wanawake katika Mji wa Sake ulioko Goma.
Taarifa
hizo zimeeleza kuwa askari mmoja wa JWTZ alihitaji kujamiiana na
mwanamke mmoja(Kahaba) kwa ujira wa Dola 50. Baada ya kumaliza shida
zake ambazo ilielezwa alizifanya bila kinga yoyote,askari huyo alikataa
kumlipa ujira wake,hali iliyoleta tafrani na mwanamke huyo kupiga
kelele.
Mtu
anayeonekana kuwa chini ya Ulinzi alikuwa ni mshiriki wa Kanali Mohamed
Bacar ambaye aliondolewa madarakani.
“Vilevile
picha hiyo ilitolewa vile vile katika tovuti za
www.apc.net.au/news/stories ya Machi 26, 2008 na ww.
Seattletimes.com.
na pia picha hiyo ipo pia kwenye tovuti ya Jamii Forum baada ya kufanya
‘link’ kutoka kwenye Mtando wa www.google.com.”
Taarifa
hiyo ilisema kuwa JWTZ inapenda kueleza wananchi na dunia kwa ujumla
kwamba wanaoneza taarifa hizo wana lengo la kukatisha tamaa juhudi
zinazofanywa na
nchi za Maziwa Makuu na SADC kuleta amani nchini DRC
kwani JWTZ wako DRC kwa mujibu wa taratibu za kiutendaji za Umoja wa
Mataifa.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment