BAADHI
ya wananchi wa mkoani MOROGORO wameshangaza na kitendo cha waunguzi
wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro,kupokezana kuwashika madripu ya
dawa wagonjwa waliolaza chini ya wodi za hospital hiyo ya rufaa nya
mkoa wa Morogoro baada ya kukosa vitanda.
.
Skendo zinazidi kuiandama hospital
hiyo ambayo imepandishwa hadhi ya kuwa hospital ya rufaa hivi karibuni
ambapo ljumaa iliyopita mtangazaji wa Top redio ya mkoani hapa Edward
Abed Mganga aliyevamiwa na majambazi na kukimwizwa kwenye hospital hiyo
imeilalamikia hospital hiyo kwakumtelekeza bila kumpa huduma kwa zaidi
ya masaa matano na kuladhimika kuondoka kwenye hospital hiyo ya serikali
na kwenda kutibiwa hospital za watu binafsi.
Mtandao huu umeibua Skendo
nyingine ndani ya hospital hiyo baada ya kushuhudia waunguzi wa hospital
hiyo wakipokeza kuwashikia madripu ya dawa wagonjwa waliolazwa chini
ya sakafu baada ya hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha.
Juzikati
hospital hiyo ilivamiwa na majeruhi zaidi ya 60 waliopoteza fahamu
baada ya kiwanda cha kutengeza nguo za michezo cha Mazava kukumbwa na
shoti ya umeme na kukimbizwa kwenye hospital hiyo,hivyo uongozi wa
hospital hiyo baada ya kuelemewa na wingi wa majeruhi hao ulilazimia
kutoa magodoro stoo na kuwalaza chini baadhi ya majeruhi hao kufuatia
hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha.
" Hii ni aibu kubwa kwa hospitali ya
rufaa ya mkoa kuwalaza chini wagonjwa hata kama wakijitetea kwamba
wagonjwa wamekuja kwa mkupo. hospital inapopewa hadhi ya rufaa inamaana
inamudu kukabiliana na majanga yoyote kwa maana wa kuhudumua majeruhi
zaidi ya mia watakaofika kwa mkupuo kwenye hospital hiyo"alisema Bi Asha
Abdallah aliyekuwepo ndani ya wodi namba 3 walipolazwa majeruhi hao.
Vile vile mwandishi wa matandao
huu mbali ya kushudia wauguzi hao wakipokezana kuwashikia madripu
wagonjwa hao pia walishuhudia wahudumu hao wakilazimika kupita juu ya
wagonjwa waliolazwa kwenye eneo la njia za wodi hizo
Ili kupata ufafanuzi wa jambo
hilo Mtandao huu ulimsaka Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo kwa zaidi ya
siku tano na kufanikiwa kumpata leo asubuhi ambapo alipotakiwa kueleza
hali hiyo Mganga huyo mfawidhi Bi Rita Lyamuya alikuwa na haya ya
kusema
" Nikweli siku ile ya tukio la
kiwanda cha Mazava tulitoa magodolo stoo na kuwatandikia chini baadhi ya
majeruhi .kiukweli kwa ishu kama ile tulikosa namna ya kukabiliana
nayo kwani walikuja kwa mkupua zaidi ya majeruhi 65 hivyo tulichofanya
tuliwapokea na baadhi kuwalaza chini na kuwapatia hudumu ya kwanza huku
tukitafuta sehemu muafaka ya kuwalaza"alisema Dr Rita
dustanshekidele blog
No comments:
Post a Comment