Kamishna Mkuu wa haki za
binadamu katika Umoja wa Mataifa,Navi Pillay, amelaani mashambulizi
mabaya yaliyofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino nchini
Tanzania ikiwemo mauaji ya mtoto mvulana.
Serikali inapaswa kukomesha mauaji hayo pamoja na unyanyapaa dhidi yao , alisema Bi Pillay.Watu watano pekee wameshtakiwa mahakamani nchini Tanzania, tangu mwaka 2000 kwa mauaji ya maalbino.
Takriban wengine 72 waliuawa katika kipindi hicho.
Mnamo mwaka 2009, rais Jakaya Kiwete, alisema kuwa mauaji hayo yaliiletea Tanzania aibu kubwa na kulazimu nchi hiyo kufanya kampeini ya kitaifa ili kukomesha dhulma hizo dhidi ya maalbino.
Mnamo mwaka 2010, Salum Khalfani alikuwa mtu wa kwanza mwenye ulemavu huo kuchaguliwa kama mbunge nchini Tanzania.
Bi Pillay alisema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wana haki ya kuishi kama mtu yeyote ule bila hofu ya kuuawa au kubaguliwa.
Katika taarifa yake, Bi Pillay alisema kuwa mashambulizi manne ya watanzania wenye ulemavu wa ngozi, yaliripotiwa katika siku kumi na sita kati ya mwezi Januari na Februari.
Ni pamoja na mauaji ya mtoto mwenye miaka saba, Lugolola Bunzari. Watu walimvamia walikata paja la uso, mkono wake wa kulia , bega la kushoto.
Babu ya kijana huyo, mwenye umri wa miaka 95, pia aliuawa kwenye shambulizi hilo, alipojaribu kumuokoa mjuu wake.
Bi Pillay alisema mashambulizi kama haya ni mabaya na watu wana haki ya kuishi kama watu wengine bila hofu ya kuuawa au kujeruhiwa vibaya.
No comments:
Post a Comment