KIJANA Peter Bosco mkazi wa Itiji,
mjini Mbeya aliyedaiwa kumuua kwa kumchoma kisu kifuani mgoni wake
Daniel Mwasalemba Februari 8, mwaka huu, naye amefariki dunia baada ya
kupigwa kwa mawe na watu wenye hasira kali.
Kwa mujibu wa ndugu wa Peter
ambaye hakutaka kuandikwa jina lake aliyezungumza na gazeti hili,
marehemu alifariki baada ya kupata majeraha kadhaa siku anayodaiwa kuua
kutokana na kupigwa kwa mawe na watu hao.
“Watu wenye hasira kali walimpiga
kwa mawe Peter siku ya tukio na kusababisha polisi wampeleke hospitali
alikolazwa baada ya kuumia, amefariki hivi karibuni na tayari
ameshazikwa,” alisema ndugu
huyo.
Peter anadaiwa kumuua Daniel kwa
kumchoma kisu kifuani na kumburuta marehemu hadi kando ya barabara huku
akiwa uchi wa mnyama baada ya kumfumania na mwanamke wake aitwayeElizabeth Michael.
Elizabeth
ambaye ni maarufu kwa jina la Lulu wa Mbeya ambaye
kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, ACP Diwani Athmani,
ni muuza pombe za kienyeji katika klabu iitwayo Musoma iliyopo Itiji,
Mbeya.
Kamanda Diwani alisema chanzo
cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya Peter kumfuma Daniel akiwa
nyumbani kwa mwanamke huyo ambapo aliwafungia mlango kwa nje na kwenda
kutafuta kisu alichokitumia kumuua mwenzake.
No comments:
Post a Comment