Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na maafisa mbalimbali wa ubalozi wa
Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole
jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria
hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na
Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete,
kabla ya kurejea Dar es salaam jana, alikwenda Uganda kuhudhuria
mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta,
aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake Rwakitura.
Balozi
wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati)
na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete
wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo jana jioni ya Februari 24,
2013.(PICHA NA IKULU).
By Freddy Maro, Rwakitura, Western Uganda
Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete jana ameungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika
kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais Yoweri Museveni
wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.
Rais
Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa
Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa
Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Akitoa
salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa
Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na
kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na
kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea
marehemu.
Rais
Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo
alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuithamini elimu ambapo
aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali
kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee
wengi wenye umri wake(97).
Rais
Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao
ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa
kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe
akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana
na changamoto nyingi katika maisha yao.
Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda.
Rais
Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha
waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo.
No comments:
Post a Comment