WAKATI
kukiwa na taarifa kwamba maofisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani
(FBI) wametua nchini kwa ajili ya kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri
Evarist Mushi, Jeshi la Polisi limetangaza dau la Sh10 milioni kwa
atakayefichua aliyemuua padri huyo.Padri Mushi aliuawa kwa
kupigwa
risasi Jumapili iliyopita wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la
Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Ras nje kidogo ya mji wa Zanzibar,
ambapo inadaiwa kuwa waliomuua walikuwa wamepanda pikipiki aina ya Vespa
na walimfyatulia padri huyo risasi tatu akiwa ndani la gari yake.
Wakati
polisi wakitangaza dau hilo, Sheikh Ali Khamis Ali (65) mkazi wa Kitope
Kaskazini Unguja, aliuawa jana kwa kukatwa mapanga mjini Zanzibar, baada
ya wezi kuvamia shambani kwake.
No comments:
Post a Comment