KASI
ya kuzuia ukwepaji kodi za Serikali uliofanywa kwa kipindi cha miezi mitatu na
utawala wa Rais Dk. John Magufuli kwa ‘kutumbua majipu’ umeokoa wastani wa Sh
bilioni 700.
Katika
utawala wa Serikali iliyopita ya awamu ya nne, wastani wa makusanyo ya kodi kwa
kiwango cha juu kwa mwezi yalikuwa Sh bilioni 900, lakini baada ya kuingia kwa
awamu hii kumekuwapo na ongezeko la zaidi ya Sh bilioni 700 kwa miezi mitatu ya
Desemba hadi Februari.
Akitangaza
ongezeko hilo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, alisema katika kipindi cha
Desemba 2015, pia TRA iliweza kuvuka lengo kwa kukusanya kiasi cha zaidi ya Sh.
trilioni 1.4 sawa na ongezeko la wastani wa Sh. bilioni 490 kwa mwezi.
Alisema
kiasi hicho ni kikubwa kikilinganishwa na wastani wa makusanyo kwa mwezi Julai
hadi Novemba mwaka jana ambapo ilikuwa ni Sh. bilioni 900 kwa mwezi. Like page
yetu ya facebook Jambo Tz