Katika Bunge hilo, wajumbe wengi wa CCM walimshambulia Warioba na tume
yake wakidai kuwa Rasimu ya Pili ya Katiba haikuzingatia maoni ya
wananchi na Mabaraza ya Katiba. PICHA|MAKTABA
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
amewashauri wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na CCM kuacha
kuzunguka mikoani kufanya mikutano inayoeleza misimamo yao kuhusu
mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa haina tija kwa taifa.
Ameonya kuwa mikutano hiyo inajenga mwelekeo mbaya
kwa taifa na kuhatarisha mchakato wa Katiba na kuzitaka pande hizo
kumaliza tofauti zao.
Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika
Dar es Salaam jana, Warioba alisema: “Kwa mustakabali mwema wa taifa,
ni muhimu makundi haya ‘ya-resolve’ (yamalize), matatizo yaliyopo kabla
ya Agosti, ili Bunge Maalumu la Katiba likirejea, wote washiriki na
kukamilisha mchakato wa kupata Katiba Mpya. Hili ni kwa masilahi ya
taifa.”
Kauli ya Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia
aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu, imekuja huku makundi ya Ukawa linaloundwa
na wabunge wengi wa upinzani na viongozi wa CCM wakiendelea
kung’ang’ania misimamo yao kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa
kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Wakati CCM ikipinga mapendekezo ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu uliomo kwenye Rasimu, Ukawa unaunga mkono mapendekezo hayo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz