Askari mwenye cheo cha sajini katika Gereza la Ruanda na polisi
mwenye cheo cha konstebo katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Mbeya,
wamekamatwa kwa tuhuma za kushirikiana na watu wengine watatu, kwa
kuteka gari na kupora fedha na mali katika eneo la Mlima wa Kawetere,
Barabara ya Mbeya-Chunya, juzi jioni.
Inadaiwa kuwa katika tukio hilo, watuhumiwa walipora Sh3.5 milioni na mabegi yaliyokuwa na vitu mbalimbali.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kushiriki katika kupora
mali ya mfanyabiashara Sheedhar Paupeleti (38) baada ya kuteka gari
alilokuwa akisafiria akiwa na watu wengine wawili.
Habari zilisema katika tukio hilo, dereva wa gari hilo Ezekiah Matatira, alifungwa pingu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,
alisema majambazi hayo yalikamatwa baada ya polisi kwenda katika eneo
la tukio, kutokana na taarifa zilizotolewa na wananchi kwa njia ya simu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz