JEURI ya pesa. Ndicho unachoweza
kusema baada ya klabu tajiri Ulaya, Paris Saint-Germain na Manchester
City kudaiwa kuwa zipo tayari kumng'oa, Lionel Messi, kutoka Barcelona
kwa gharama yoyote ile.
Wakati ikiwekwa wazi kwamba thamani ya
supastaa huyo wa Kiargentina ni Euro 400 milioni, klabu hizo
zinazomilikiwa na matajiri wenye pesa ndefu, zimesema zipo tayari.
Ripoti zinabainisha kwamba uamuzi wa
kumfanyia tathmini Messi ili kufahamu thamani yake halisi, umefanywa
mahususi na klabu hizo ili kufahamu itawagharimu kiasi gani ili kuipata
saini yake. Kwa mtazamo wa kawaida anaonekana mchezaji huyo ni kama
hanunuliki.
Kwa mujibu wa tathmini hiyo
iliyofanywa na klabu tatu za Ulaya zenye pesa za kutosha, staa huyo wa
Barcelona na mshindi mara nne wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia (Ballon
d'Or), thamani yake ya sasa inazidi kipengele kilichowekwa kwenye
mkataba wake kwamba anaweza kuuzwa kwa Euro 250 milioni.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Profesa Gerardo Molina, aliyeandika
ripoti kuhusu thamani ya mwanasoka huyo, alisema: "Kuna klabu
zinazothaminishwa na serikali (zimeripotiwa kuwa PSG na Man City)
zinajiandaa kulipa Euro 400 milioni kwa ajili ya Lionel Messi.
"Kuna klabu tatu za Ulaya zilituuliza
sisi tufanye tathmini ya thamani ya mchezaji huyo ili kufahamu ni
kiwango gani kinahitajika kumnasa Messi. Hatuwezi kuzitaja klabu hizo,
lakini kitu ambacho zinataka ni kumhamisha Messi."
Molina aliongeza: "Messi soko lake ni
mara tano ya Cristiano Ronaldo. Kwa tathmini iliyofanywa, Ronaldo
thamani yake ni kati ya Euro 150 milioni na Euro 160 milioni. Mkataba wa
Messi una kipengele cha Euro 250 milioni, lakini kiwango hicho
hakikutazama thamani yake halisi.
"Kwa sasa hakuna mchezaji mwingine
duniani mwenye thamani kubwa kuliko Messi. Kwa uchunguzi uliofanywa
kwenye soka la usajili kwa miaka mitano, Messi thamani yake ni zaidi ya
Euro 400 milioni."
Staa huyo juzi Jumapili alikuwa
jukwaani wakati klabu yake ilipomenyana na Elche kwenye mchezo wa Ligi
Kuu Hispania na Barcelona kushinda mabao 4-0, Alexis Sanchez akifunga
'Hat-Trick' kuisaidia timu hiyo kuendelea kuongoza msimamo wa ligi hiyo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment